Hakika usipo staajabu ya Musa basi yatakustaajabisha ya Firauni!!....katika hali isiyokuwa ya kawaida mwajiri mmoja aliyefayiwa kitendo cha uhalkifu na mfanyakazi wake ameamua kubandika tangazo la kumsaka Mtumishi wake huyo kwa udi na uvumba kwa kubandika Tangazo hilo katika Lori la Mafuta tofauti na wenzake wafanyao hivyo katika Magazeti na televisheni.
Pichani ni Lori hilo la Mafuta T 718 BUK kama lilivyonaswa na Mdau wa Blog hii ya Father Kidevu, Balozi Patrick Lusiano Tsere, maeneo ya Kibamba huku mtafutaji akiahidi donge nono la Dola za Kimarekani 2000 kwa atakae mnasa mwizi wake.
0 comments:
Post a Comment