Nafasi Ya Matangazo

July 21, 2012

Maji wa EPIQ BSS wakiwa wamesimama kimya kwa dakika mbili ili kutoa heshima kwa watu waliopoteza maisha katika ajali ya Boti ya MV Skagit iliyozama juzi huko Zanzibar kabla ya kuazan kwa usaili wa vijana watakao shiriki shindano hilo kutoka Mkoani Mbeya ambapo zoezi linafanyika kwa siku mbili Julai 21-22, 2012 katika ukumbi wa CLUB VYBES mjini Mbeya. Majaji hao kutoka kushoto ni  Salama Jabir, Madam Ritha,  Masta J na Meneja Mawasilino wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Awaichi Mawala.
 Vijana kibao wa mjini Mbeya wamejitokeza kuwania nafasi ya kuwakilisha mkoa huo katika shindano la EPIQ BSS mjini Mbeya na hapa ni vijana waliofika Club Vybes katika usaili wakibandika namba zao.
 Baadhi ya washiriki waliojitokeza katika usaili huo wakiwasikiliza maelekezo kutoka kwa wasimamizi kabla ya kwenda mbele ya majaji.
 Vijana wakijipanga mistari kwenda kupokea namba na huku wengine wakiondoka baada ya kupata namba zao na wanasubiri kwenda kushuka mistari yao kwa majaji.
Meneja Mauzo wa Zantel mkoani Mbeya, Agrey Mwakilema  nimiongoni mwa watu kibao waliojitokeza kuchangia damu, zoezi ambalo limepokelewa vyema na vijana waliojitokeza katika usaili huo siku ya kwanza hapa Club Vybes.
 Majaji sasa waliingia kazini na hapa wapo makini kumsikiliza mmoja wa washiriki katika usaili huo. Kutoka kushoto ni Master J, Madam Ritha na Salama Jabir. Kazi ilikuwa ngumu maana zaidi ya vijana 600 leo tu walijitokeza sijui kesho itakuaje.
 Vijana wakiwa nje wakisubiri kuingia katika mchujo.
 Huyu kwa leo amevunja rekodi ya Mkoa wa Mbeya ni mshiriki mdogo kuliko wote aliyeingia katika usaili kutoMbeya na anaenda kwa jina la GOODLUCK BROWN. Akina Dogo Janja kibao mwaka huu huenda wakapatikana kama hawa wa Mbeya
 Huyu ni Amina Rashid kwa leo yeye ndio alikuwa mshiriki wa kwanza kuingia kwa Majaji kwa usaili mkoani Mbeya.
 Jamaa ana swaga za kiaina na anakwenda kwa jila la Martin Steven Chiwale, mshiriki wa EPIQ BSS kutoka Mbeya.
Posted by MROKI On Saturday, July 21, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo