Leo mchana hali ya hewa ya Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam ilibadilika ghafla na kuwa ya harufu kali inayonuka kupindukia baada ya mafundi wa Kampuni ya Simu nchini TTCL kuanza kumwaga maji machafu barabarani ambayo yanadaiwa kuchanganyika na maji ya chooni.
Maji hayo yalikuwa yakimwagwa kutoka katika moja ya Chemba zilizopo jirani na Mnara wa Askari na jingo la IPS. Mafundi hao wanadai waliamua kumwaga maji hayo yaliyo jaa katika chemba yao kiasi cha kushindwa kufanya kazi ya matengenezo.
Lakini baadhi ya wapiti njia na wenye biashara kando ya mtaa huo, waliiambia Father Kidevu Blog kuwa ni vyema wangetafuta gari la kunyonya maji machafu likafanya kazi hiyo kistaarabu zaidi kuliko njia mabayo wameitumia ya uchafuzi wa mazingira.
0 comments:
Post a Comment