Nafasi Ya Matangazo

June 08, 2012

Picha ni Mh.John Mnyika akiwa katika vijiji vya Kata za Makukwe na Mkwedu, wilayani Newala. Kwa George Mkuchika ambako alikutana na kiashiria cha wazi kuhusu udhaifu wa Waziri Mkuchika (Mbunge wa Newala) katika kusimamia majukumu yake, baada ya wananchi katika Kijiji cha Tengulengu, Kata ya Mkwedu kumlalamikia kuwa Diwani wa Kata hiyo, Juma Dadi hajawahi kufungua ofisi yake zaidi ya mwaka mmoja sasa. Pamoja na kuwasilisha malalamiko yao kwa barua Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala na kwa Mbunge wao, Mkuchika, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Pichani ni Mwenyekiti Freeman Mbowe akikata utepe wa kufungua Ofisi ya CHADEMA Kijiji cha Mkangaula. Ilikuwa ni baada ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa kutoa hotuba ya ufunguzi na John Mnyika kupandisha bendera ya chama nje ya ofisi hiyo, ikiwa ni ishara ya kupiga hatua katika mapambano ya awamu ya pili.Picha zingine zinamuonesha Mnyika akitoa 'somo' kwa wanakijiji wa vijiji vya Kata ya Lumesule. Mapema kabla alikaribishwa na kuzungumza na Katibu wa Tawi wa CUF, Bi. Zaituni (pichani). Wananchi walimwelewa vyema. Kadi zikauzwa vizuri. Akaacha uongozi wa muda wa tawi lenye wanachama wa 34. Katika Kijiji hicho cha Lumesule, mwananchi mmoja kwa jina la Yasin Mohamed alihoji ilikuwaje CHADEMA wakaachia Dkt. Slaa ashindwe urais, wakati alichaguliwa kwa kura nyingi na wananchi na wao wanajua alishinda uchaguzi huo wa mwaka 2010.
Mbunge wa jimbo la Ubungo (CHADEMA) John Mnyika akipandisha bendera ya chama nje ya ofisi ya CHADEMA Kijiji cha Mkangaula
Mh Freeman  Mbowe akihutubia mara baada ya kufungua tawi kwenye moja ya kijiji walichofanya mkutano wao.
 Akina mama wakishangilia  PIPOOOOOOOOOOZ POWER
 Sehemu ya umati wa watu kwenye mkutano huo
Opresheni Okoa Kusini katika picha, hapa ilikuwa Masasi Mjini. Waweza kuona katika baadhi ya picha watu walivyopanga mstari kupigania kadi

Posted by MROKI On Friday, June 08, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo