Nafasi Ya Matangazo

June 22, 2012

Deidre Lorenz na Rais wa IBF-USBA bala la Africa, Masharini ya Kati na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi.

Mcheza sinema toka Marekani Deidre Lorenz amewasili mjini Moshi tayari kushiriki kwenye mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika juni 24. Lorenz amwasili leo na ndege ya Ethiopian Airlines ambao ndio wafadhali wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zinazofanyika jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita kila mwaka.

Ujio wa Lorenz ambaye amecheza sinema nyingi zikiwamo Santorini Bule, Perfect Strangers, The Big Fight umeleta msisimko mkubwa katika mji huu mkuu wa Kilimanjaro. Ujio wake umefuatia matayarisho ya muda mrefu ambayo yanaendana na hadhi yake.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kumshuhudia mcheza sinema huyu, Lorenz alisema kuwa ameisikia kuwa mlima wa Kilimanjaro uko Kenya kwa kwa muda mrefu na ana furaha kubwa sana ya kufika ili kushughudia kuwa mlima huu maarufu duniani uko Tanzania. “Nimekuwa nautangaza sana ujio wangu kwenye blog na tovuti yangu, wapenzi wangu pamoja na watu wengi wanangojea kurudi kwangu nikawaambie niliyoyashughudia” alisema Deidre Lorenz ambaye ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kwa tuzo za Oscar. Lorenz alisema kuwa kwa miaka mingi alifikiri kuwa mlima Kiliamnjaro uko Kenya kwa jinsi nchi hiyo jiraniminavyoutangaza nchini Marekani.

“Sasa nimeona mwenyewe kwa macho yangu kuwa kweli mlima (Kilimanjaro) huu maarufu duniani uko Tanzania na sio Kenya” alisema Deidre Lorenz ambaye anaishi kwenye jiji la New York City linalofahamika kama jiji la pesa (International Financial Capital) la kimataifa. Lorenz ameshukia katika hoteli ya Bristol Cottages iliyopo karibu na benki ya Standard Chattered mkabala na bustani ya Manispaa ya Uhuru Park.
Posted by MROKI On Friday, June 22, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo