Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akicheza kuashilia ufunguzi rasmi wa mashindano ya wazi ya mchezo wa vishale (Tanzania Intarnational Open Darts Championships) kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni,ajira na michezo jijini Mwanza jana.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa, Gesase Waigama.
MASHINDANO ya Vishale ya Wazi jijini Mwanza yamefunguliwa rasmi leo na Meneja wa Bia ya Safarai
Lager kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni ,Ajira na Michezo ambaye alipata ajali akielekea kwenye ufunguzi huo.
Akizungumza na wachezaji mejeja alisema Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imekuwa ikidhamini mashindani ya vishale kwa muda sasa kwa kutambua umuhimu wa mchezo huu kwa wapenzi na mashabikmi kwa ujumla na itaendelea kudhamini mchezo huu katika mashindano mbalimbali ya ndani na yale ya kimataifa ili kuinua mchezo huo.
Shelukindo alisema Darts ni moja ya michezo ambao inatakiwa ipewe kipaumbele kama michezo mingine kama Safari Lager inavyoudhamini mchezo huu unaofanyika katika Hoteli ya Monarch jijini Mwanza kwa siku nne ambapo mashindano hayo ya Afrika Mashariki yanatarajiwa kufikia tamati mwishoni mwa wiki hii kwa kushirikisha nchi nne Tanzania,Kienya , Uganda na Rwanda.
Alusema Shelukindo a kuwa katika mashindano hayo ya Afrika mashariki,TBL kupitia bia yake ya safari imetoa fedha kiasi cha shilingi milioni 32 kwa ajili ya kugharimia mashindano hayo,ambapo pia wametoa medali pamoja na fedha taslimu kwa ajili ya washindi wa kwanza hadi wanne.
Amesema kuwa pamoja na kudhamini mashindano hayo kwa mwaka wa tatu mfululizo TBL pia imetoa vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuchezea mchezo huo katika amshindano ya mwaka huu.
’’Pia TBL kupitia bia yake ya safari imeamua kuboresha vifaa vya kuchezea mchezo huo vilivyopo katika ameneo mbalimbali hapa nchini,mara nyingi mchezo huu umekuwa ukifanyika katika mazingira ya baa,hivyo kutoa udhamni ni kurejesha mchango wetu kwa watumiaji wa bia yetu ya safari’’,alisema.
Mwenyekiti wa chama cha darts(TADA)Gesase Waigama aliipongeza kampuni ya bia Tanzania kupitia bia yake ya safari kutokana na kutoa udhamini mnono wa michuano hiyo ya Afrika mashariki mwaka huu.
Waigana alisema kuwa mchezo wa darts unakabiliwa na tatizo la vifaa kuuzwa kwa bei ya juu na ni mara chache kwa mchezaji kuweza kununua vifaa hivyo hivyo udhamni unaotolewa umekuwa ukiwakomboa wachezaji wa mchezo huo.
Mwenyekiti huyo wa TADA alisema kuwa mashindanoi ya mwaka huu yanatarajiw akuwa na ushindani mkubwa toka kwa nchi wanachama wa afrika amshariki kutokana na namna timu hizo zilivyojiandaa mwaka huu.
Pamoja na kuipongeza TBL kutokana na kutoa udhamini huo,Mwenyekiti huyo aliwataka wadhamini wengine kujitokeza kwa wingi kudhamini michuano hiyo katika siku zijazo.
0 comments:
Post a Comment