Nafasi Ya Matangazo

June 19, 2012

 Mchakato wa kuendelea kuitambulisha huduma ya Airtel Supa5 mikoani utaendelea mwishoni mwa wiki hii ambapo Airtel itaweka kambi mkoani Mwanza katika viwanja vya wazi vya furahisha vilivyopo jijini Mwanza. 

Akizungumzia tamasha hilo la kuitambulisha SUPA5 mkoani Mwanza Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde  alisema lengo la kuunganisha utambulisho huu burudani ni kuwavutia vijana na wateja wengi kuhudhuria na kujifunza faida lukuki za SUPA5 ili waitumie zaidi

Tamasha linafanyika kwa siku mbili mfululuzizo ambapo siku ya jumamosi tunatoa fulsa kwa wasanii chipukizi kujitokeza kwa wingi kuonyesha vipaji vyao sambamba na  kupata huduma ya Airtel SUPA5

Jumapili itakuwa uzinduzi kamili ambapo wasanii wakubwa watatoa burudani BURE, akiwemo Juma Nature na kundi zima la wanaume halisi, Mwasiti a.k.a SOJA, Roma Mkatoliki a.k.a mzee wa tuzo kibao watatoa burudani kali kwa wateja watakaohuduria tamasha hilo BURE


 Bi Matinde pia amezungumzia lengo la huduma ya  dili tano bomba zilizopo kwenye huduma ya SUPA5 kuwa Airtel inatimiza dhamira yake iliyojiwekea ya kufikisha na kupunguza gharama za mawasiliano nchini kote bila kuwasahau vijana na  wanafunzi kunufaika kwa kupata internet bure wakati wa usiku, kutuma sms bure na faida nyingine nyingi.

Huduma ya Airtel SUPA5 ilizinduliwa rasmi siku za karibuni jijini Dar es salaam kisha kufuatiliwa na kufanyika kwa matamsaha ya burudani ya BURE katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Iringa, Arusha huku mwishoni mwa wiki hii itakuwa zamu ya wakazi wote wa Mwanza

Wasanii mahiri waliokwishapamba majukwaa ya Airtel SUPA5 hadi sasa kwa mkoa wa Dar es salaam ni Fid Q, Mwasiti, Godzilla, pamoja na Kundi la Tip Top Connection akiwemo Madii, Tundaman,Richard na Dodo Janja kwa mkoa wa IRINGA ni  Juma Nature na kundi zima la wanaume halisi,Roma mkatoliki, pamoja na Kundi la Tip Top Connection akiwemo Madii, Tundaman na Richard. Mkoa wa Morogoro na Dodoma ni kundi mahiri la Wanaume family likiongozwa na Chege na Temba na kukamilisha ladha ya zaidi kwa kuwepo kwa  Bendi Maarufu jijini ya Mashujaa band ikiongozwa na kingunge Charles Baba na wasanii wengine.


Posted by MROKI On Tuesday, June 19, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo