Meneja wa bia ya Balimi Edith Bebwa kushoto akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa mashindano ya ngoma za asili ya balimi yanayotarajiwa kuanza kwenye mikoa ya kanda ya ziwa june 30 kulia ni meneja masoko wa Tbl Fimbo Buttal.
********
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager, leo imezindua rasmi mashindano ya ngoma za asili ya Balimi Extra Lager kwa mwaka 2012. Mashindano haya ambayo yametokea kupendwa sana na wakazi wa kanda ya ziwa yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika mikoa mbali mbali ya kanda ya ziwa kuanzia Juni 30.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam, meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Bi. Edith Bebwa alisema; Bia ya Balimi Extra Lager imekuwa ikiendesha mashindano haya maarufu kama “Mashindano ya Ngoma za Asili ya Balimi Extra Lager” kwa zaidi ya miaka saba sasa , na kwa kweli napenda kusema kuwa ni mashindano yaliyotokea kupendwa sana katika kanda yetu hii ya ziwa,
Lengo kuu la kudhamini mashindano haya ni kushirikiana na wakazi wa kanda ya ziwa katika kuenzi na kulinda tamaduni za kanda alisema Bi Edith .
Kwa mwaka huu wa 2012, mashindano yataanza rasmi tarehe 30 Juni katika ngazi za mikoa na kumalizika tarehe 21 Julai. Tutaanza na mkoa wa Mwanza ukifuatiwa na mikoa ya Mara, Kagera, Shinyanga na Tabora, katika mpangilio ufuatao.
Tarehe
| Mkoa | Viwanja |
30/06/2012 | KAGERA | Kaitaba |
07/07/2012 | MWANZA | Ccm Kirumba |
14/07/2012 | TABORA | Chipukizi |
21/07/2012 | SHINYANGA | Shycom |
21/07/2012 | MUSOMA | Bwalo la Magereza |
28/07/2012. | FINALS MWANZA | Ccm Kirumba |
Akielezea juu ya zawadi za mwaka huu, bi. Edith Bebwa alisema; kama ilivyo ada ya Bia ya Balimi, kila mwaka tumekuwa tukiongeza zawadi ili kuongeza chachu ya ushindani na kuleta tija kwa washindani. Kwa mwaka huu tumeongeza zawadi kwa takribani asilimia 20 ukilinganisha na mwaka jana. Hii yote inaonesha jinsi gani bia ya Balimi inatambua, inajali na kuthamini utamaduni wa kanda yetu. Zawadi kwa washindi ni kama ifuatavyo;
| Ngazi ya mkoa | Finali |
Mshindi wa kwanza | 600,000 | 1,100,000 |
Mshindi wa pili | 500,000 | 850,000 |
Mshindi wa tatu | 400,000 | 600,000 |
Mshindi wa nne | 300,000 | 500,000 |
Mshindi wa tano hadi wa kumi kila kikundi | 150,000 | 250,000 |
Pamoja na zawadi hizi nono, pia Balimi Extra Lager itaendelea kutoa huduma muhimu kwa vikundi shiriki kama vile chakula na malazi. Tunaamini kabisa mambo yote haya yataongeza hamasa na msisimko katika mshindano ya mwaka huu. Na kauli mbiu yetu kwa mwaka 2012 “Balimi Extra Lager, twajivunia utamaduni wetu”.
Akizungumzia maandalizi ya fainali hizo, Meneja Masoko wa Tbl Fimbo Buttalah alisema; Maandalizi yote kwa upande wetu sisi wadhamini yameshakamilika, hivyo niwaombe tu washiriki wote ambao nimepata taarifa kuwa wamekuwa mazoezini kwa muda sasa, waendelee na mazoezi ili kuonesha uwezo wa juu utakaoleta ushindani na kutoa burudani yenye kiwango cha juu.
Kwa niaba ya bia ya Balimi Extra Lager, tunapenda kuwakaribisha watu wote kuhudhuria mashindano haya ambayo tarehe na mahali yatakapofanyikia zitakuwa zikitangazwa redioni ili waweze kushuhudia burudani hii na kuuenzi utamaduni wetu. Pia wananchi wasisahau kuwa katika burudani hizi pia wataburudika na Bia yao waipendayo ya Balimi Extra lager baridi, na kushinda zawadi mbali mbali katika promosheni za Balimi zitakazoambatana na Mashindano haya ya Ngoma za asili ya Balimi Extra Lager.
0 comments:
Post a Comment