Mkali
wa Bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond akiimba jukwaani hii leo wakati
wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika uwanja wa Kirumba
jijini Mwanza leo.
Barnaba
Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimbo jukwaani hii leo
wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika
Uwanja wa Kirumba leo.
Msanii
AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza sho wake wakati wa show
maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika Uwanja wa Kirumba
leo
Barnaba akipiga picha kwa staili yake
Diamond akiwa juu katika machuma ya Jukwaa
Vijana wa Kazi wa Diamond wakiwajibika
Roma Mkatoli akishusha mistari
Isha Mashauzi akifanya vitu vyake
Ben Paul nae akikimbiza
Omy Dimpoz nae alifanya vitu vyake
DJ Choka akimsindikiza Roma Mkatoliki
Mashabiki wakifuatilia show
Huyu ni Diamond wa Mwanza akiongoza show ya mashabiki
Mashabiki walifurika
******
WASANII wa Musiki wa Kizazi Kipya
Diamond, Roma, Isha Mashauzi, AT, Barnaba, Omy Dimpoz, Ben Paul wamefunika
vibaya katika Tamasha la Kili Music Award Winners Tour lililofanyika katika
Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza, na kutoa burudani ya uhakika kwa wapenzi wa
burudani ya Musiki wa jiji hilo na vitongoji vyake.
Show hiyo kali iliyoanza majira ya saa 8
mchana ikitanguliwa na makundi kadhaa ya wasanii chipukizi wa Bongo Fleva wa
Jijini Mwanza ilizidi kupamba moto muda hadi muda hadi pale wasanii Nguli na
washindi wa Tuzo za Kili Music Award 2012 walkipowasili uwanjani hapo.
Katika kukuza vipaji na kuibua vipaji
vipya vya wasanii chipikizi Msanii Christian Joachim maarufu kama Christian JJ
alifanikiwa kuwashinda wenzake wawili akiwepo mwana dada kutoka Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Augustino cha Jijini Mwanza Bertha Denis.
Christian JJ aliibuka kidedea baada ya
kupata kura nyingi za mayowe zilizo lipuka kutoka kwa mashabiki takribani wote
uwanjani hapo na kuungana na mshindi mwingine kutoka mkoani Dodoma ambao
wataenda jijini Dar es Salaam kurekodi nyimbo yao moja kwa Mtayarishaji wa
Muziki maarufu.
Alianza jukwaani kupanda mwanadada wa
Kikurya anaeimba Taarabu, Isha Mashauzi wa Mashauzi Clasic ambaye alijinyakulia
Tuzo ya Wimbo bora wa taarabu kupitia
wimbo wa Nani kama Mama na
kukonga nyoyo za wapenzi wa taarabu vilivyo kwa kuimba vibao vyake kadhaa.
Isha Mashauzi alifuatiwa Jukwaani na mshindi
wa Tuzo ya wimbo Bora wa R&B.
Msanii
Ben Paul ambaye alijinyakulia tuzo hiyo kupitia kibao Number One ambapo nae
alishambulia jukwaa vilivyo.
Omy Dimpoz alifuata jukwaani kwa kuimba
nyimbo zake kadhaa ikiwapo ile iliyo mpa tuzo ya Wimbo bora wa Kushirikishwa ya
Nai Nain a kusindikizwa na wacheza show wake wanne.
Mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji bora wa
Kiume, Barnaba alifuata jukwaani na kuimba nyimbo kadhaa na kumpisha Mkali
kutoka Zanzibar ambaye ni mshindi wa Tuzo Wimbo Bora wenye Vionjo vya Kiasili
AT ambaye aliimba nyimbo kadhaa ikiwepo iliyompa Tuzo ya Vifuu Utundi amabyo
aliicheza vilivyo na wanenguaji wake waili wa kike.
Baada ya Kushika AT alipanda tena
Barnaba kasha kumpisha Mkali wa Tuzo za Kili Music Award 2012 Diamond ambaye
alijizolea Tuzo tatu alipanda jukwaani kwa kishondo huku akiwatanguliza wacheza
show wake.
Diamond akishangiliwa vilivyo aliimba
sambamba na kucheza nyimbo zake takriban zote huku zilizo mpa tuzo za Wimbo
Bora wa Mwaka na ule wa Mawazo uliompa Tuzo bora ya Video bora zikishangiliwa
vilivyo.
Diamond ambaye ndiye anazungumzwa kwa
sasa kuwa msanii ghali na bora nchini alimudu vyema kushambulia jukwaa na
kuwafanya mashabiki muda wote mikono kuwa hewani.
Pazia la Wasanii washindi wa tuzo za
Kili Music Award 2012 wanaofabnya ziara na waliobahatika kufika jijini Mwanza
lilifungwa na Roma Mkatoliki a.k.a Mpare wa
milimani aliyeshambulia jukwaa kwa nyimbo zake kadhaa za mistaari ya maandiko.
Roma
ambaye ni Mshindi wa tuzo mbili za Wimbo Bora wa Hip Hop kupitia wimbo wake wa
Mathematics na Tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop, alishambulia jukwaa huku
viitikio vyake vikiimbwa na DJ Choka.
Wasanii
hao wiki ijayo wanataraji kutoa burudani kama hiyo Mkoani Kilimajaro katika mji
wa Moshi na tayari walisha tumbuiza na kuwashukuru mashabiki wao wa Mkoani
Dodoma kwa kuwapa kura za ushindi.
0 comments:
Post a Comment