Nafasi Ya Matangazo

May 04, 2012

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi waliangua Vicheko pale wenzao wa CHAMADA walipoikwepa kuigusa nakuila Keki ya Birthday ya Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shy Rose Banji wakati wa tafrija yake iliyofanyika Nyumbani Longe Jijini Dar es Salaam.

Wabunge hao wa CHADEMA  ni Halima Mdee (Kawe) ambaye anaonekana picha ya juu akiikataa keki hiyo iliyotolewa na Wakurugenzi wa Nyumbani Longe, Gadna G Habash na Mkewe Lady Jay Dee, huku Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Kiwelu picha ya chini nae akijificha asiitazame kwa karibu.
 
Wabunge hao waliigwaya Keki hiyo kutokana na jinsi ilivyopambwa rangi za CCM.

Huku Wabunge wa CCM wakishangilia wakimtaka Halima Mdee aongoze Ukataji wa Keki hiyo ambayo ilitolewa baada ya keki ya awali iliyoandaliwa na Baby Girl Shy Rose kuliwa, ilishindikana kuliwa na kuhifadhiwa.
 
Watu mbalimbali walihudhuria tafrija hiyo ndogo wakiwepo Wabunge, wanasiasa, Wasanii musiki, Watangazaji na Wanahabari ambapo kila aliye simama kuongea alimpongeza sana Shy Rose kwa kuwa Mpambanaji wa Ukweli katika kutafuta kile anachotaka na kumuombea kwa Mungu amuongoze vyema katika kazi yake.

Posted by MROKI On Friday, May 04, 2012 4 comments

4 comments:

  1. AnonymousMay 04, 2012

    sasa mlienda tafuta nini kama sio unafiki?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2012

    yaani kweli CCM kwishney,nilidhani hawa wabunge wa CHADEMA tu ndiyo walisusa kumbe hadi ilishindikana kuliwa ikahifadhiwa? na wewe jaydee kwani hiyo ilikuwa siku CCM ilpozaliwa? mnaona mlivyomfedhesha mwenzenu?

    ReplyDelete
  3. MZEE wa ndekuleMay 05, 2012

    mh huu c o uungwana siasa kazini uku urafik,kila kitu kina mipaka au ukila utakuwa umekula BENDERA

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2012

    Hawana lolote hao,wanaitamani sana.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo