· Punguzo la SMS la 45% hadi Tsh. 25 kwa SMS kwenda mtandao wowote Tanzania.
· Kurambaza mitandao ya Facebook na Twitter bure
· Simu za wateja wa Vodacom wa malipo ya kabla zitajisajili moja kwa moja kwenye ofa hii
Dar es Salaam, Mei 7, 2012: Vodacom
leo imezindua ofa mpya ya kusisimua iliyoandaliwa hususan kukidhi
mahitaji ya mawasiliano ya umma wa soko la vijana ili kuendelea kukuza
idadi yake ya wateja kwa kutoa huduma za mawasiliano ya simu yanaomudika
kwa Watanzania wote.
Katika kampeni mpya iitwayo Wajanja wateja
wa Vodacom wa malipo ya kabla watatozwa kiwango cha chini kabisa cha
robo shilingi kwa simu za Vodacom kwenda Vodacom kuanzia saa 4 usiku
hadi saa 1 asubuhi. Ofa hii mpya vile vile itawatoza bei ya chini kabisa
ya ujumbe mfupi ya Tsh 25 kwenda mtandao wowote Tanzania, pamoja na kurambaza tovuti ya Facebook na Twitter bure.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza alisema ofa hii mpya
imeandaliwa kukidhi mahitaji ya walio wengi katika soko la mawasiliano
la simu za mkononi, hususan vijana- na itawawezesha kuwa na taarifa
motomoto kila wakati na kuwawezesha kuwasiliana kwa simu za sauti,
ujumbe mfupi na Intaneti kwa bei wanazozimudu. Hakika vijana si vijaba
tu watakaofurahia ofa hii mpya bali wateja wote wa Vodacom wa huduma ya
kulipia kabla watafaidika na huduma pamoja na viwango hivi vipya vya
chini.
“
Vodacom imenuia kutoa huduma kwa bei ambazo Watanzania wote wataweza
kuzimudu. Kwa kuwawezesha Watanzania kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi na
kutumia Intaneti kwa bei nafuu, tunaamini kwamba wateja wa simu za
mikononi wa Tanzania sasa wataweza kuwa sehemu ya dunia ya kisasa
kupitia simu zao za mkononi, “ alisema Meza.
Ofa
hii haihitaji wateja wa huduma za kulipia kabla kujisajili. “ Hakuna
haja ya wateja kujisajili kwenye ofa hii. Watafaidika ili mradi wako
hewani kwenye mtandao wa Vodacom”, Meza alisema.
“
Tukiwa na wateja hai wapatao milioni 20, sawa na 44% ya soko la simu za
viganjani, soko la Tanzania linatoa fursa kubwa ya kukua kwa biashara,
fursa ambayo Vodacom inataka kushiriki kikamilifu huku tukiendelea
kuongoza soko la simu za mkononi kwa kutoa huduma za bei ambazo wateja
watazimudu”, Meza alimalizia.
Mwamvita Makamba
Ofisa Mkuu wa Mahusiano na Mauzo
kwa Wateja Wakubwa
0 comments:
Post a Comment