Bi Emelda Taikwa Adam, Afisa
Mazingira mwandamizi kutoka Ofisi ya makamu wa Rais Akiwasilisha maoni ya
Tanzania katika masuala ya Kilimo na mabadiliko ya Tabia nchi, katika mkutano
wa sayansi ya Taaluma ya mabadiliko ya tabia nchi unaendelea mjini Bonn
Ujerumani (Picha na Evelyn Mkokoi)
Washiriki Kutoka Tanzania
kulia Bi Fauzia Haji kutoka Idara ya Mazingira Zanzibar,Katikati Bi Imelda Adam
Afisa Mazingira mwandamizi Ofisi ya Makamu wa Rais, na Bw. Ladslaus Kyaruzi
Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamo wa Rais wakijiandaa
kuwasilisha mada kwa niaba ya nchi za Africa katika mkutano wa Sayansi na
Taaluma ya Mabadiliko ya Tabia Nchi unaendelea Mjini Bonn Ujerumani kuhusu
Madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.
**********
Na EVELYN MKOKOI ,BONN
UJERUMANI
Tanzania kama nchi nyingine
zinazoendelea imepata fursa ya kuwasilisha maoni yake kuhusu kilimo katika
kuhimli mabadiliko ya Tabia nchi katika mkutano kimataifa wa 36 wa sayansi na
taaluma ya mabadiliko ya tabia nchi, unaendelea mjini Bonn Ujeremani.
Akiwasilisha maoni hayo,
katika Mkutano huo Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya makamu wa Rais Bi
Emelda Taikwa Adam ameeleza kuwa, nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania
zinatakiwa kuangalia zaidi katika kuhimili mabadiliko ya tabia nchi ili kuweza
kuongeza uzalishaji na kuhakikisha usalama wa
chakula kupitia sekta ya
kilimo kwani ndo uti wa mgongo wa Taifa.
Bi Emelda aliongeza kuwa,
katika kuhimili mabadiliko ya Tabia nchi Tanzania kupitia sekta ya kilimo na
tafiti zilizokwisha fanyika kuonyesha kuwa kuna matumizi salama ya mbegu
zinazohimili ukame, pamoja na matumizi sahihi ya kilimo cha umwagiliaji, na
kuna kila sababu ya matumizi ya teknolojia zaidi ya kisasa na kujenga uwezo kwa
wakulima wa kawaida ili kuweza kuhakikisha usalama wa chakula.
“Tafiti zinaonyesha kuwa
kilimo huchangia 13% katika kuzalisha gesi joto hivyo basi kuna umuhimu mkubwa
wa kuingiza masuala ya kilimo katika kuhimili mabadiliko ya tabia nchi, kwa
sababu nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hutegemea kilimo alisisitiza.”
Akizungumzia athari za
mabadiliko ya Tabia nchi katika sekta ya kilimo bi Emelda amesema kuwa,
kupungua kwa mvua kunakopelekea ukame nchini na kuongezeka kwa gesi joto
kumeathiri kwa kiasi kikubwa sana sekta ya kilimo, na katika kupunguza gas joto
katika kilimo kunahatarisha usalama wa chakula na kupoteza ardhi kwa wenyeji.
Aliongeza kuwa pamoja na
kwamba sekta ya kilimo imekuwa na mikakati mbalimbali inayotekelezeka katika
kuhimili mabadiliko ya tabia nchi, Tanzani inatakiwa kuwa na mfumo ambao
utahakikisha kuwa upunguzaji wa gesi joto katika kilimo unatokana na jitihada
za kuhimili mbadiliko ya tabia nchi.
0 comments:
Post a Comment