Nafasi Ya Matangazo

May 17, 2012

 Balozi wa Denmark nchini Bw. Johnny Flento akiweka mzigo katika mzani ili kuweka uwiano sawa kama ishara ya uzinduzi wa Mfuko wa Msaada wa Huduma za Kisheria (Legal Services Facility) leo (Alhamisi, Mei 17, 2012) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bi. Angela Kairuki, Jaji Mkuu wa Zanzibar Bw. Omar Makungu na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Bw. Semstocles Kaijage.
 Meneja wa Mfuko wa Msaada wa Huduma za Kisheria (Legal Services Facility)Bw. Kees Groenendijk akitoa maelezo kuhusu mfuko huo katika hafla ya uzinduzi wake jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Mei 17, 2012) kwa viongozi waliohudhuria. Kutoka kushoto: Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Bi. Joaquine De Mello Balozi wa Denmark nchini Bw. Johnny Flento, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bi. Angela Kairuki, Jaji Mkuu wa Zanzibar Bw. Omar Makungu na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Bw. Semstocles Kaijage.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bi. Angela Kairuki akiweka mzigo katika mzani ili kuweka uwiano sawa kama ishara ya uzinduzi wa Wengine kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Bi. Joaquine De Mello, Balozi wa Denmark nchini Johnny Flento, Jaji Mkuu wa Zanzibar Bw. Omar Makungu na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Bw. Semstocles Kaijage.
Kikundi cha Kwaya cha Jaji Mwalusanya kikitumbuiza katika uzinduzi wa Mfuko wa Msaada wa Huduma za Kisheria (Legal Services Facility) leo (Alhamisi, Mei 17, 2012) jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Farida Khalfan wa Wizara ya Katiba na Sheria).


Na Farida Khalfan
Serikali inandaa muswada wa Sheriaitakayosimamia shughuli za utoaji huduma za msaada wa kisheria zinazofanywa naMawakili Jamii (paralegals).

Naibu Waziri wa Katiba na SheriaBi. Angela Kairuki ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 17, 2012) wakati akizinduaMfuko wa Msaada wa Huduma za Kisheria jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwapamoja na kazi nzuri wanayofanya, wanahitaji msaada wa uratibu kisheria.

Mfuko huu unalenga kuboreshaupatikanaji wa haki hususan kwa wanawake, watoto na watu wanaoishi katikamazingira magumu na ni sehemu ya msaada wa Serikali ya Denmark kwa Tanzaniakatika kuboresha sekta ya sheria.

Naibu Waziri huyo alisema Serikalikupitia Tume ya Kurekebisha Sheria ilifanya utafiti wa kina kuhusu matumizi yaMawakili Jamii katika utoaji wa huduma za kisheria ikiwemo kuwawakilishawananchi katika Mahakama.

“Ninafurahi kuwataarifu kuwaSerikali imepokea taarifa ya utafiti huo hivi sasa inaifanyia kazi kwa lengo lakuwa na sheria itakayowatambua na kuwasimamia Mawakili Jamii (Paralegals)nchini”, alisema Naibu Waziri.

Kairuki alisema uwepo wa sheriahiyo utaongeza upatikanaji wa haki kwa wananchi wengi zaidi kwa kuwa MawakiliJamii ni watu wenye elimu ya kawaida na wanapatikana kwa wingi zaidi zaidinchini kote ikilinganishwa na wanasheria.

Pamoja na uandaaji wa sheria hiyo,Naibu Waziri aliyashukuru mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwa kazi kubwawanayofanya ya kutoa msaada wa huduma za kisheria kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Kairuki, wananchiwengi kutoka makundi maalum wamekuwa wakipata msaada kutoka katika mashirikahaya.

“Wanafanya kazi nzuri sana. Watuwengi wakiwemo wajane, yatima, walemavu na hata wale wanaoishi na virusi vyaukimwi wanategemea msaada kutoka katika mashirika haya,” alifafanua.

Akimkaribisha Naibu Waziri katikahafla hiyo, Balozi wa Denmark nchini Bw. Johnny Flento alisema mfuko huounaofadhiliwa na serikali ya Denmark una lengo la kujenga na kuboresha uwezo wawatoa huduma za msaada wa kisheria nchini ili kuongeza upatikanaji wa haki.

Kwa mujibu wa Balozi Flento,mafanikio waliyoyapata katika kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotoahuduma za msada wa kisheria, yameitia moyo Serikali yake na kuifanya kukubalikufadhili uanzishwaji wa mfuko huo.

“Uzoefu wetu umeonyesha kuwamsaada wa kisheria na Mawakili Jamii wana ushawishi mkubwa katika kuongezauwezo wa wananchi kudai na kulinda haki zao na hivuyo kuboresha upatikanaji wahaki,’ alisema Balozi Flento.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodiya Mfuko huo Bi. Joaquine De Mello alisema kwa kuanzia, mfuko huo utajikitakatika mambo matatu.

Aliyataja mambo hayo kuwa nikuongeza wigo wa msaada wa kisheria katika wilaya zote nchini; kuboresha uborawa msaada wa kisheria unaotolewa na kuboresha uratibu katika utoaji wa msaadawa kisheria katika ngazi zote.
Posted by MROKI On Thursday, May 17, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo