Nafasi Ya Matangazo

February 19, 2026









Na. Sixmund Begashe, Rombo
Wananchi wanaoishi kuzunguka Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro wamatakiwa kuendeleza uhifadhi na kutunza mazingira kwani hali hiyo imesaidia hifadhi hiyo kuwa ya pili Kitaifa kwa kuingiza mapato mengi hatua itakayochochea maendeleo kutokana na fedha zinazotokana na Utalii pamoja na uhifadhi. 

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameyasema hayo katika mkutano wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba na wananchi wa Wilaya ya  Rombo, Mkoani Kilimanjaro na kubainisha kuwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ndio inayoshika nafasi ya kwanza kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni na mapato makubwa kwa ujumla. 

Dkt. Kijaji amefafanua kuwa kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza Utalii na uhifadhi endelevu, sambamba na kuboresha miundo mbinu katika hifadhi za Taifa imepelekea  Hifadhi hiyo kuingiza shilingi bilioni 364,733,948,036 katika kipindi cha kuanzia februari 2022 hadi 2026. 

Katika suala la kupambana na Wanyamapori wakali na waharibifu hususani Tembo na Tumbili, Dkt. Kijaji amewahakikishia wananchi hao kuwa Wizara anayoiongoza itaendeleza jitihada za kukabiliana na madhara yanayosababishwa na Wanayamapori hao kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo  kwa njia mbalimbali ikiwemo teknolojia za kisasa. 

Aidha amewapongeza wananchi hao, kwa kuendelea kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika Uhifadhi endelevu wa Hifadhi hiyo yenye vivutio adimu duniani ukiwemo Mlima wa Kilimanjaro, kwa kuwa, faida yake ni kubwa kama vile ajira hasa kwa vijana.
Posted by MROKI On Thursday, February 19, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo