Meneja Kampeni wa Simba SMS, Talib Rashid kutoka kampuni ya Push Media Mobile akichezesha bahati nasibu ambayo shabiki wa Simba kutoka mkoa wa Arusha, Abubakari Hassan alishinda piki piki yenye thamani shs Milioni. 1.8.Wengine katika picha ni Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga na Msimamizi wa michezo ya Kubahatisha kutoka body ya michezo hiyo nchini, Bakari Maggid.
Mwandishi wetu
SHABIKI wa timu ya soka ya Simba mkoani Arusha, Abubakar Hamis ameibuka kidedea katika droo ya bahati nasibu katika kampeni ya changia simba inayoendeshwa kwa ushirikiano baina ya Kampuni ya Push Mobile Media na klabu ya Simba.
Katika bahati nasibu hiyo Hamis ambaye ni dereva taxi amejinyakulia zawadi ya pikipiki yenye thamani ya zaidi ya shilingi milion tatu.
Kwa mujibu wa Meneja Kampeni wa Simba sms, Talib Rashid shabiki huyo ni miongoni mwa mashabiki zaidi ya 40 wa klabu hiyo kongwe hapa nchini waliojishindia zawadi mbalimbali ikiwamo pesa taslimu.
"Droo kubwa itafanyika Julai na mshindi atajinyakulia bajaji," alisema Rashid na kuongeza mashabiki wanatakiwa kuandika neno Simba na kutuma kwenda 15678 kuingia katika bahati nasibu hii.
Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema ushindi wa shabiki huyo ni uthibitisho tosha kwamba mashabiki wao wanashinda katika bahati nasibu hiyo.
"Naomba wanachama na mashabiki wetu wajitokeze kushiriki katika bahati nasibu hii kwani ni moja ya kuichangia klabu ya Simba iweze kujiendesha na kufanya vizuri zaidi ndani na nje ya Tanzania," alisema Kamwaga.
Mshindi atazawadiwa zawadi yake ndani ya wiki mbili kuanzia sasa na kampuni ya Push Mobile Media itagharimia gharama za usafiri na kulala wakati wa kuja hapa jijini.
Alisema kuwa kwa sasa wamebakiza piki piki moja na bajaj ambazo drow yao itachezeshwa siku moja.
0 comments:
Post a Comment