Nafasi Ya Matangazo

May 23, 2012

Precision Air mdhamini rasmi wa safari ya Mustafa Hassanali.
Mustafa Hassanali ashiriki maonyesho ya mavazi kwa mara ya tatu mjini Kampala,Uganda.

Mbunifu nguli wa mavazi Afrika Mashariki na Kati Mustafa Hassanali amepokea mualiko maalum kutoka kwa mbunifu mashuhuri nchini Uganda, Bi Nambi Brenda anaemiliki lebo ya mavazi ya B’ambi Designs, kushiriki katika maonyesho ya mavazi ya East Afica Fashion Extravangaza, yatakayofanyika tarehe 26 Mei katika mji wa Kampala nchini Uganda. Baada ya kuonyesha katika maonyesho makubwa ya mavazi ya Arize Magazine Fashion Week mjini Lagos, Nigeria mwezi Machi 2012, Mustafa Hassanali atazindua rasmi nguo zake mpya ziitwazo Afrikalos katika onyesho hili.

“Nina furaha kubwa ya kuonyesha mavazi yangu kwa mara ya tatu mjini Kampala na Kudumisha mahusiano yaliyopo kati ya Uganda na Tanzania.” Alisema Mustafa Hassanali.

Kwa mara ya kwanza Mustafa Hassanali alionyesha mavazi yake mjini Kampala katika uzinduzi wa kwanza wa wiki ya mitindo ya Uganda mwaka 2003 na baadae mwaka 2006 alionyesha mavazi yake katika maonyesho binafsi la mbunifu maarufu wa mavazi nchini Uganda Sylivia Owori. Mwaka huu safari ya Mustafa hassanli imedhaminiwa na Precision Air ambalo ni shirika kubwa la ndege nchini Tanzania ambao linafanya safari zake kwenda mjini Entebbe mara sita kwa wiki.

 “Precision Air ni mfano wa kuigwa kwani imechangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya wajasiriamali wengi, na imetoa mchango mkubwa katika tasnia ya ubunifu wa mavazi na mitindo. Na ninashukuru kwa kuniwezesha kufika mjini Kampala na kuonyesha kipaji changu”. Alimaliza Hassanali.

Licha ya kuwa ameonyesha mavazi yake katika nchi 15 na miji 24 ulimwenguni kwote, pia Mustafa Hassanali jina lake lipo katika orodha ya wabunifu 10 bora wa kiume ya Jarida la NEW AFRICAN WOMANI la nchini Uingereza. Pia aliteuliwa na waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo kuwa mjumbe katika kamati maalum ya Tanzania ya kupendekeza vazi  la taifa.

Ama kwa hakika Mustafa Hassanali alizaliwa na kipaji maalum.
Kwa maelezo tafadhali tembelea www.mustafahassanali.net
Posted by MROKI On Wednesday, May 23, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo