Katibu Tawala Msaidizi - Mkoa wa Mwanza Bw. Ndaro
Kulwijila wa pili kutoka kushoto (waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja
na Mafundi Mchundo wa Majokofu na viyoyozi kutoka katika
viwanda mbalimbali vya jiji la Mwanza waliohudhuria mafunzo ya njia bora
za hifadhi ya tabaka la Ozoni. Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya
Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wakufunzi kutoka VETA Mwanza na VETA
Kigoma.
Katibu Tawala Msaidizi - Mkoa wa Mwanza Bw. Ndaro
Kulwijila akifungua mafunzo kwa mafundi Mchundo kuhusu njia bora za
kuhudumia majokofu na Viyoyozi na umuhimu wa kuhifadhi tabaka la Ozoni.
Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na
yanafanyika Jijini Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya Mafundi Mchundo wa Majokofu na Viyoyozi kutoka viwanda mbalimbali vya Jiji la Mwanza wakisikiliza kwa makini umuhimu wa kuhifadhi tabaka la Ozoni
0 comments:
Post a Comment