Nafasi Ya Matangazo

May 05, 2012

 Ilikuwa kama ndoto lakini ni kweli yalitimia, tunaamini kimwili hauko nasi lakini kiroho tunakukumbuka daima mpendwa wetu. Upendo wako kwa familia hautasahaulika kamwe na hakuna wa kuliziba pengo.

Ni miaka 11 sasa imepita tangu ulipotutoka  mpendwa wetu dada Lucy S. Wambura (Mama Luca), Unakumbukwa daima na mama yako kipenzi Mama Lucy (Annastazia) na wadogo zako wote Dory, Grace, Theo, Tinna, Pendo na Anna  wanoa Mr, Iddi, Jacky, Luca, Josepha (Kurwa) na Joan (Doto).

Kutakuwa na Misa ya kumwombea marehemu  siku ya Jumamosi tarehe
 05-05-2012 katika kanisa la Parokia ya bikira Maria mama wa huruma Mbezi Beach-Tanki Bovu saa 12:30asubuhi na baada ya misa kutembela nyumba ya milele alipolala mpendwa wetu Lucy, Makaburi ya kinondoni.
Wote mnakaribishwa.

Raha ya milele umpe eeeh bwana na mwanga wa milele umuangazi apunzike kwa amani – Amina
Posted by MROKI On Saturday, May 05, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo