Mchezaji
wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza Quinton Fortune,
akikabidhi moja ya madawati yaliyotolewa na Kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maarifa Mareitha
Mulyalya huku Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Elimu), Mh Kassim Majaliwa akitazama. Kampuni ya Airtel Tanzania ilitoa
mipira 30, jesi seti tatu na madawati 40 kwa shule za msingi za
Maarifa, JICA na Mwangaza zote za Gongo La Mboto, Dar es Salaam.
Mchezaji
wa zamani wa Manchester United ya Uingereza Quinton Fortunewa pili
kulia, akionyesha waandishi wa habari (hawako pichani) baadhi ya vifaa
vya michezo vitakavyotumika kwenye michuano ya soka ya kimataifa kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars jana kwenye
Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam. Kati ni Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Technologia Mh. Professa Makame Mbarawa, wa kwanza kulia ni
Mkurugenzi Mashindano wa TFF Sandy Kawembe, Mkurugenzi Mtendaji wa
Airtel Tanzania Sam Elangallor na Mkurugenzi Bidhaa Airtel Afrika Obina
Justine.
Mchezaji
wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza Quinton Fortune,
akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa michuano ya vijana wenye umri
chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars. Uzinduzi huo ulifanyika jana,
Mei 10, kwenye Hoteli ya Sea Clif, jijini Dar es Salaam.
Msanii
wa kizazi kipya Ambwene Yesaya maarufu kama AY, akiwatumbuiza wanafunzi
wa Shule ya Msingi ya Maarifa iliyopo Gongo La Mboto nje kidogo Jijini
Dar es Salaam wakati Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ilipotoa
msaada wa madawati 30, mipira ya miguu 40 na jezi seti tatu, Alhamisi
Mei 10, 2012 ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri kwenye Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa (Elimu) Mh. Kassim
Majaliwa. Shule zingine zilizofaindika na msaada ni Maarifa, JICA na
Mwangaza zote za Gongo La Mboto, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment