Mkurugenzi
mtendaji wa New Habari Corporation Bw. Hussein Bashe (kushoto)
akimpigia simu mshindi wa zawadi ya gari aina ya Vitz kwenye shindano
la Jishindie mchongo Bw. Kassim Ramadhani mkazi wa eneo la Kunduchi
mtongani jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia) na Meneja
mauzo wa kampuni hiyo Bw. Godbless Urassa (katikati)
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi
akizungumza na mhariri mtendaji wa kampuni ya New Habari Corporation
wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa, na The
African Bw. Prince Bagenda (katikati) mara baada ya kuwasili katika
ofisi za kampuni hiyo kushuhudia utoaji wa zawadi mbalimbali likiwemo
gari lenye thamani ya shilingi milioni 8 kwa wasomaji walioshiriki
bahati na sibu ya Jishindie Mchongo leo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi
akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kutembelea
chumba cha habari cha New Habari Corporation wachapishaji wa magazeti ya
Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa, na The African . Kutoka kulia ni Bw.
Prince Bagenda mhariri mtendaji na Mkurugenzi mtendaji Bw. Hussein
Bashe.
Mratibu
wa shindano la Jishindie mchongo lililowahusisha wasomaji wa magazeti
ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa na The African Bw. Essu Ogunde
akichanganya karatasi zilizojazwa na wasomaji tayari kwa kuchagua
mshindi wa zawadi ya gari aina ya Vitz lenye thamani ya shilingi milioni
8 leo jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (katikati) na Mkurugenzi
mtendaji Bw. Hussein Bashe.
Wafanyakazi wa New Habari Corporation wakifuatilia kwa makini fainali za shindano hilo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akiangalia gari atakayokabidhiwa mshindi shindano la Jishindie Mchongo lililoandaliwa na kampuni ya New Habari Corporation wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa, na The African leo jijini Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment