Mkulima wa Mpunga mkazi wa Mlali Wilayani Mvomero akipandikiza miche ya Mpunga katika shamba lake lililopo Kijiji cha Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali wilayani humo leo.
Msimu wa Kilimo cha Mpunga kwa baadhi ya maeneo unazidi kushika kasi Mkoani Morogoro hususani Wilayani Mvomero, na wakulima wanaendelea na zoezi la kupandikiza mpunga mashambani licha ya kutokuwepo kwa mvua za kutosha na maji kwaajili ya ukuaji wa zao hilo kwa baadhi ya mashamba.
Pichani ni Mmoja wa wakulima wa zao hilo ambae ni Mkazi wa Mlali, Wilayani Mvomero mkoa wa Morogoro, Ashura Alli akipandikiza (kugombeka) mpunga katika moja ya shamba lake lililopo Kijiji cha Kipera.
Ashura anadai uhaba wa mvua unaolikabili eneo hilo unawawia viguu wakulima wengi kushindwa kulima mwaka huu na hata walio lima mashamba yao hayana maji jambo ambalo linaashiria upatikanaji wa Mpunga na chakula kwa ujumla kuwa mgumu maeneo hayo ya Tarafa ya Mlali na vitongoji vyake.
Aidha mwandishi wa Blogu hii alishuhudia baadhi ya mashamba mengi ya Mpunga yakiwa hayajalimwa hadi hivi sasa na baadhi ya watu waliopanda Mahindi yakianza kunyauka kutokana na ukame kiasi cha kupoteza matumaini kwa wakulima.
0 comments:
Post a Comment