Nafasi Ya Matangazo

April 21, 2012

Siasa ni kitu kizuri sana hasa kikitumiwa kwa malengo yanayotakiwa na hasa katiika kuleta maendeleo, daima wanasiasa huwa na malumbano na kuoneshana chuki wanapokuwa katika mambo mengi ya kutafuta maendeleo ya wananchi wao na taifa kwa ujumla. Juzi Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alizua hoja ya kutafuta saini 70 za kumuondoa Waziri Mkuu madarakani zoezi ambalo linadaiwa kukamilika hadi sasa. 

Mtu mwingine anaweza sema kwa kauli ile huenda sasa Pinda na Zitto wakawa ni maadui lakini hakika ile ni siasa na mambo ya siasa ni siasa na urafiki na ujamaa wao upo pale pale kama hivi wanavyoonekana katika picha hii iliyopigwa leo mjini Dodoma nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma 

Pichani za juu zinamuonesha  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge, John Mnyika wa Ubungo (kushoto), Kabwe Zitto wa Kigoma Kaskazini  na Hamad Rashid wa Wawi, kwenye jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma Aprili 21, 2012.

lakini huku mtaani washabiki wa siasa hizo saa ingine wanaumizana, kuchukiana na kushindwa kusikilizana kwa namna yeyote ile. 
Posted by MROKI On Saturday, April 21, 2012 1 comment

1 comment:

  1. Siasa ni mchezo ambao kama hujui kucheza acha... mimi nawasiwasi sana na mawaziri wanaotuhumiwa kuwa na kinyongo pinda acha acheke maana upole umemzidi hata kama hakushiriki kuwateua hao mawaziri basi angemwambia baba mkubwa sitaki kazi

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo