HABARI zilizotufikia
hivi punde kutoka Mjini Dodoma zinasema kuwa wakati wowote kutoka sasa Mawaziri zaidi ya watano katika Baraza
la Mawaziri la Rais Jakaya Kikwete huenda wakajiuzulu hii leo.
Taarifa hizo ambazo
bado hazijawa rasmi zinatoka mjini humo na kuwataja mawaziri zaidi ya watano
kuamua kuchukua uamuzi huo mgumu kufuatia lawama nyingi zinazoendelea kulikumba
baraza hilo.
Mawaziri waliotajwa
hadi sasa kutaka kujiuzulu hii leo ni pamoja na Waziri wa Niashati na Madini,
William Ngeleja, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ciril Chami, Waziri wa Afya
na Ustawi wa jamii, Dk. Haji Mponda, WAZIRI wa Uchukuzi, Omar Nundu na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Prof. Jumanne
Maghembe.
Blog hii
itaendelea kukupa taarifa kamili juu ya hili na mengine mengi.
Ni muda muafaka sera ya kung'ang'ania uongozi ufike kikomo. Uzalendo unadhihirika kiongozi au anaeongozwa kuachia muelekeo potofu na ikilazimika kwa vielelezo au dhamira kuachia ngazi ya uongozi au muelekeo wa kupotosha au kuipeleka jamii pabaya. Hawa watu wajiuzulu. Hatua kama hii itaidhihirishia umma kwa ujumla kwamba uongozi ni Utumishi siyo kutumia!
ReplyDelete