Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Balozi wa Korea nchini, Young-Hoon Kim, wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha VETA kilichojengwa Mkoa wa Lindi. uzinduzi huo ulifanyika jana Aprili 10, 2012. Kulia ni Mkurugenzi wa VETA, Zebadia Moshi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyeza 'Alam', kuashiria uzinduzi rasmi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha VETA kilichojengwa Mkoa wa Lindi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA baada ya kuzindua rasmi chuo hicho kilichojengwa Mkoa wa Lindi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Shukuru Kawambwa, Balozi wa Korea nchini, Young-Hoon Kim na Viongozi wa VETA, wakati akitembelea na kukagua baadhi ya Majengo mapya yaliyojengwa ya Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA, baada ya kuzindua rasmi chuo hicho mkoa wa Lindi jana Aprili 10, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Ghariub Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu jinsi ya ufundishaji wanafunzi kwa kutumia mtambo wa kufua Umeme, kutoka kwa Mwalimu wa Umeme Veta, Majolo Mwigole, wakati Makamu alipofika kuzindua Chuo hicho cha VETA mkoa wa Lindi jana Aprili, 10, 2012.
0 comments:
Post a Comment