Nafasi Ya Matangazo

April 13, 2012

 KAVA LA NJE LA KITABU HICHO KINACHO MZUNGUMZIA MAREHEMU KANUMBA
HUU NI UKURASA WA MWANZO KABISA UNAPO FUNGUA KITABU HICHO

*******
KATIKA HALI ISIYO YA KAWAIDA MUDA HUU MAENEO YA UBUNGO KUMEIBUKA MAUZO YA NAKALA MOJA YA KITABU AMBACHO KINAMUELEZEA MAREHEMU KANUMBA NA MAMBO MENGINE, KITABU  HICHO AMBACHO MPAKA TUNAPO RIPOTI MUDA HUU ENEO LA TUKIO KINAUZWA NA WATU WENGI SANA WANANUNUA KWA KIASI CHA SHILINGI ELFU TATU PEKEE.

PIA IKUMBUKWE MAREHEMU NI JUZI TUU AMEZIKWA MSIBA UNAENDELEA LAKINI WATU KUPITIA MGONGO WA MAREHEMU WANAFANYA BIASHARA HIYO YA KUUZA COPY HIZO

MSEMO HUU KWELI UPO? KUFA KUFAANA! JE  TABIA HII NANI ALAUMIWE NANI AIKOMESHE? kwa hisani ya Mdau Tony wa Darblog

WAKATI HUO HUO

SHIRIKISHO  la Filamu Nchini (TAFF), limesema litamchukulia mtu yeyote hatua za kisheria atakayebainika kuuza CD za shughuli za mazishi ya marehemu Steven Kanumba bila ridhaa ya familia.

Tamko hilo lilitolewa jana na Rais wa TAFF, Simon Mwakifamba katika mkutano wake na waandishi wa habari, nyumbani kwa marehemu Sinza Vatican jijini Dar es Salaam ambapo lengo lao ilikuwa ni kutoa salamu za shukrani kwa wote waliohudhuria msiba huo.

Mwakifamba alisema tayari wameshapata taarifa za watu kuanza kuuza cd hizo kwa lengo la kujipatia fedha jambo ambalo sheria ya filamu hairuhusu.

Kwa mujibu wa Rais huyo, Kanumba alikuwa akitegemewa na familia yake kupitia kazi za filamu ambapo sasa hivi kutokana na kutokuwepo kwake familia itayumba.

Hivyo alisema endapo CD hizo zitaweza kusimamiwa vizuri pato lake litaingia kwenye familia na kuweza kuendesha maisha yao ya kila siku badala ya jasho hilo kufaidiwa na watu wengine.

Kwa upande mwingine alisema msiba wa Kanumba ni pigo kwa tasnia ya filamu kutokana na namna msanii huyo alivyoweza kuitangaza  Tanzania kupitia kazi zake.

Mwakifamba alisema TAFF itamkumbuka kwa mambo mengi,kwani mbali na kuwa mwanachama kupitia chama cha Waigizaji Kinondoni,pia alikuwa mjumbe wa kamati ya TAFF ya kuandaa mapendekezo ya marekebisho kanuni ya sheria za filamu za mwaka 2011.

Vilevile Kanumba alikuwa ni mmojawapo ya wafadhili wa Shirikisho hilo na alikuwa na mchango mkubwa katika kuleta umoja na mapinduzi ya kweli katika tasnia ya filamu.
Posted by MROKI On Friday, April 13, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo