Nafasi Ya Matangazo

April 01, 2012

Naibu Mkurugenzi Mkuu  wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Hamis Mdee akikabidhi mashuka 150 kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Ruth Malisa wakati alipotembelea Hospitali ya Mawenzi Mkoani Kilimanjaro jana 31/3/2012. Hospitali hiyo imesajiliwa na Mfuko huo na inahudumia wanachama wa Mfuko. Mshuka hayo ni sehemu ya mashuka 700 yenye thamani ya Shilingi Milioni 7 ambayo Mfuko huo unayatoa kwa Vituo vya Afya vya Mkoa huo kama sehemu ya kuihudumia jamii katika maadhimisho ya Miaka Kumi ya Mfuko huo.

Hospitali ya Mawenzi mjini Moshi imetenga jengo maalum kwa ajili ya kuwahudumia Wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Pichani Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Hamis Mdee akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr. Kapalala Saganda ambapo alisema hii ni katika hatua za kuboresha huduma kwa wanachama hao. Sehemu hiyo ina nafasi ya vyumba vitatu vya madaktari, maabara, chumba cha dawa na vyumba vya matibabu. Alisema jambo hili limesaidia sana kuboresha huduma kwa wanachama na wamedhamiria kuendelea kuboresha huduma kwa wanachama hao.
Katika maadhimisho ya Miaka 10 ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Mfuko umekuwa ukiendelea kufanya mikutano ya wadau katika mikoa mbalimbali ya Tanzania. Pamoja na hayo Mfuko umekuwa ukitembelea viongozi wa Mikoa na Vituo vya Afya ili upata ripoti mbalimbali na kujadili uboreshaji wa huduma kwa Wanachama wa Mfuko. Pichani Naibu Mkurugenzi Mkuu  wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Hamis Mdee akiwa ameambatana na viongozi wengine wa Mfuko wakijadili mambo na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa KilimnanjaAro Bi. Ruth Malisa na viongozi wengine wa Mkoa jana katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Mfuko huo unategemea kuwa na Mkutano wa wadau mjini Moshi siku ya Jumatatu 2/4/2012.
Posted by MROKI On Sunday, April 01, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo