Nawahakikishia tukiwa na programu maalum ya utoaji elimu kuhusu utendaji na faida ya NHIF/CHF kwenye ngazi ya kata,mwitikio wa wananchi wengi kujiunga na mifuko hii hautakuwa wa kusuasua hapa Mkoan Mara ,kwani mahitaji ya huduma bora za matibabu ni makubwa zaidi hususani vijijini na CHF imejikita huko..Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda bwn. Francis Mtinga ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati ufunguzi wa kongamano la siku ya wadau wa NHF kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mara.
Mama Leticia Nyaboke akiwa amemaliza kumfunika mtoto Neema kwenye hospitali ya mkoa wa mara ambapo NHIF ilitoa msaada wa mashuka 400 kwa hospital hiyo,ikiwa ni maadhimisho ya miaka 10 ya mfuko iliyoambatana na siku ya wadau wa mkoa huo.
NA.Paul Marenga-Mara
Watendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mifuko ya Afya ya Jamii wametakiwa kuhamasisha wananchi kujiunga na mifuko hiyo kwani uelewa mdogo wa utendaji wa Mifuko hii kwenye mkoa Mara ndiyo chanzo cha kuwa na Idadi ndogo ya wanachama wachangiaji,kwani hadi disemba mwaka jana ni kati ya kaya 237,071 zilizopo ni kaya 1,460 tu zilizojiunga na CHF sawa na 0.6 %asilimia. Akizungumza Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda bwn. Francis Mtinga alisema ‘Pamoja na agizo na maombi ya bodi ya wakurugenzi wa NHIF, nawataka muandae utaratibu na kuwa na program maalum za kuwashirikisha watendaji kuanzia ngazi ya kata,kutoa elimu stahiki kuhusu utendaji wa mifuko hii,sanjari na maboresho ya huduma za afya hapa mkoani kwetu kwani wananchi wana uwezo wa kuchangia kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato walivyo navyo lakini elimu ndiyo kikwazo.
Pia amewaomba wananchi kuwa walinzi wa huduma za matibabu hususani wanapokutana na dawa zinazotolewa na serikali zinauzwa katika maduka ya watu binafsi,toeni taarifa kwa wahusika ili hatua stahili zichukuliwe,.bwn Francis Mtinga alisema.
Naye mjumbe wa bodi ya wakurugenzi NHIF ambaye pia ni Rais wa CWT bwn. Gratian Mukoba amewataka wakuu wa wilaya,waheshimiwa wabunge, makatibu tawala na watendaji kuanzia ngazi ya kata na Halmashauri, kuunganisha nguvu ya pamoja katika kusimamia fedha za NHIF/CHF ,sambamba na uhamasishaji wa wananchi kuchangia Mifuko ya Afya ya Jamii,Mikopo ya Vifaa Tiba na Ukarabati wa Majengo.
Bodi imeidhinisha mikopo hii zaidi ya miaka mitatu (3) lakini watoa huduma wengi hawajachangamkia fursa hii,hivyo nitumie nafasi hii kuwahamasisha ili kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama na wananchi kwa ujumla kwenye hospitali,zahanati na vituo vya afya vilivyopo mkoani kwenu.
Wakichangia katika kongamano hilo bwn Alfonce Mwita mtoa huduma wa kata ya kyabakari kutoka Tarime alisema watoa huduma wachache wasio na maadili wamekuwa wakidhoofisha,nia njema ya serikali kupitia mifuko hii ya NHIF/CHF katika kuboresha huduma za matibabu nchini.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeendelea kuwa na makongamano ya siku za wadau kwenye mikoa yote nchini sanjari na maadhimisho ya miaka 10, kama ambavyo umefanyika Mkoani Mara ,lengo likiwa ni kufanya mrejesho na kukusanya maoni na ushauri kwa wadau wake,ili kuboresha utendaji wake.
0 comments:
Post a Comment