Nafasi Ya Matangazo

March 13, 2012

Mwanamke mkazi wa Jijini Dar es Salaam akiwa amembeba mtoto mdogo ambaye haijajulikana kama ni wake au laa na ubebaji wa mtoto huyo haupo sahihi kwani amembeba katika hali ya kuzidi kujipatia kipato. Licfha ya jua kali kuwaka katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na kituo cha daladala Msalaba Mwekundu, mtoto huyo hajafunika lakini mwanake huyo amejifunika kichwani kukwepa jua hilo.
Mwanamke huyu akiwa katika pilika pila zake za kutafuta ridhiki kwa njia ya kuomba omba kwa wapita njia hasa katika magari.
Baadhi ya wanawake na Ombaomba mbalimbali wamekuwa wakitumia watoto ambao sio wao kwa shuguli hizi za kujitafutia kipato na kushindwa kuwabeba katika njia salama na kuwakinga na jua na mvua kama mtoto huyu. Vyombo husika havina budi kuchukua hatua kwa wazazi wa namna hii.
Posted by MROKI On Tuesday, March 13, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo