Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia chanjo dhidi ya magonjwa ya mdodo na kideri huku akipata maelezo kutoka kwa , Dk. Gabriel Shirima wa Maabara Kuu ya Mifugo ya Temeke kuzindua matokeo ya utafiti wa kuboresha ufugaji wa kuku wa asili katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo jijini Dares Salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga fimbo mfano wa umbo la yai ikiwa ni ishara ya kuzindua matokeo ya utafiti wa kuboresha ufugaji wa kuku wa asili katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo jijini Dares Salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo ya ufugaji kuku wa asili kutoka kwa mfugaji , Godfrey Mwaipopo mkazi wa Kibaha wakati wa uzinduzi wa matokeo ya utafiti wa kuboresha ufugaji wa kuku wa asili katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo jijini Dares Salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifafanua jambo katika picha ya pamoja na wadau wa uzinduzi wa matokeo ya utafiti wa kuboresha ufugaji wa kuku wa asili katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo jijini Dares Salaam.
7669 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoka kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaa baada ya kuzindua Mradi wa Ufugaji kuku wa Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Machi 28,2012. Kulia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Benedict Ole -Nangoro.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Philip Mulugo (kushoto) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukandala baada ya kufungua Mkutano wa Kitaifa kuhusu Elimu ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwenye hoteli ya Kunduchi jijini Dar es salaam Machi 28, 2012.
0 comments:
Post a Comment