Nafasi Ya Matangazo

March 22, 2012

Mwanamitindo Millen Magese (kushoto) akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo. Pamoja nae ni Mtendaji wa TAbasamu PR, Lucy Kihwele.
Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Millen Happiness Magese ataendesha zoezi la kutafuta wanamitindo wawili (kwa vijana wa kike na kiume) watakoshiriki kwa mara ya kwanza katika  maonyesho  ya wiki ya Mavazi ya Afrika Kusini (South Africa Fashion Week) tarehe 1 April mwaka huu.

Millen atafanya zoezi hilo kupitia kampuni yake ijulikanayo kwa jina la Millen Magese Group Company Limited chini ya mpango wake wa kuitangaza Tanzania kupitia fani ya mitindo (Tanzania International Fashion Exposé (TIFEX).

Alisema kuwa wanamitindo wanaotaka kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika SAFW kufika siku ya Jumapili tarehe 25 mwezi huu kwa ajili ya mchujo huo kuanzia saa 8.00 mchana kwenye hotel ya Serena.

Alifafanua kuwa anaamini kuwa wanamitindo wa Tanzania watakaopatikana katika zoezi hilo wataiwakilisha Tanzania vyema katika wiki ya maonyesho ya mavazi ya Afrika Kusini na kuitangaza Tanzania kimataifa kama anavyofanya yeye kwa hivi sasa.

Alisema kuwa hiyo ni fursa pekee kwa wanamitindo  kuweza kujitangaza wenyewe kimataifa na kufuata nyayo zake.

Alifafanua kuwa wanamitindo wanaotakiwa kufika katika zoezi lazima wawe na vigezo vifuatavyo:- Umri miaka 18 mpaka 24, urefu 1. 75m, hips 37cm (ukiwa na nywele zako za asili) na kwa wanaume urefu ni 1.82m.

“Naamini kuwa zoezi hili litawanufaisha wana mitindo wa kike na wa kiume wa Tanzania na vile vile ushiriki wao katika SAFW na katika maonyesho mengine ya mavazi nje ya Afrika na kusaidia kuitangaza nchi kimataifa,” alisema Millen.

Alisema kuwa lengo kubwa la kampuni yake ni kuendeleza fani ya uanamitindo na vile vile kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake kwa kupitia fani ya mitindo na hata kwa njia ya utalii.

Aliongeza kuwa japo Tanzania ina wanamitindo wengi na wabunifu, bado kuna pengo kubwa ukilinganisha na maendeleo ya fani hiyo katika nchi ya Afrika Kusini na Nigeria.

Alisema kuwa nchi hizo zimepiga hatua kubwa sana na yeye kuhamasika kuanzisha kampuni yake iliyozinduliwa mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kuziba pengo hilo na kuleta maendeleo ili wahusika wafaidike na matunda ya fani yao.

Majaji wa zoezi hilo ni Ritha Poulsen, Mustapha Hassanali na Khadija Mwanamboka na katika kuwekea umuhimu zaidi mchakato huo, MMG imemkaribisha mwanamitindo maarufu, Aminat  Ayinde kutoka America  Next top model cycle 12 kushuhudia zoezi hilo lililodhaminiwa na Clouds FM na Benchmark production.
Posted by MROKI On Thursday, March 22, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo