Nafasi Ya Matangazo

March 19, 2012

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia), akimkabidhi Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, tuzo maalum ya kutambua mchango wake wa kuanzisha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mwaka 2001, katika sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya mfuko huo, Dar es Salaam.
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, akifurahia tuzo maalum aliyozawadiwa baada ya kuwa msimamizi wa karibu na wa moja kwa moja wa mfuko huo katika miaka ya mwanzo hasa wakati makundi mengi yalikuwa yanapinga.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia), akizindua kitabu cha taarifa za mfuko huo vijijini zilizokusanywa na wanahabari katika mikoa mbalimbali nchini. Kushoto ni Ofisa Habari na Elimu kwa Umma wa NHIF, Grace Michael.
Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wakionesha vitabu viwili vilivyozinduliwa jana kikiwemo cha kuelezea maendeleo ya mfuko huo. Watumishi hao walishiriki kuhariri vitabu hivyo.

 Baadhi ya viongozi na watumishi wa mfuko huo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkapa
 Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wilson Mukama akipokea tuzo
 Mwenyekiti wa kwanza wa Bodi ya NHIF, Profesa  Lucian Msambichaka akipatiwa tuzo na Mizengo Pinda
 Rais mstaafu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Mjumbe mstaafu wa Bodi ya NHIF, Margareth Sitta akipatiwa Tuzo
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Said Mwema (kulia)  alikuwa ni miongoni wa viongozi waalikwa.
 Mmiliki wa Blog maarufu ya Michuzi, Muhidin Issa Michuzi, akipatiwa tuzo na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya baada ya kuwa mmoja wa mashujaa waliosaidia mfuko huo kusonga mbele
                 Michuzi akionesha tuzo hiyo. Michuzi hivi sasa ni Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais
 Faraja Kihongole wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya kwa kutambua mchango wa kihabari wa kuendeleza mfuko huo
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF, Deogratias Ntukamazina (kushoto) akipokea tuzo kwa kuendeleza vizuri mfuko huo

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya (kushoto) akimkabidhi tuzo maalum, Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Emmanuel Humba kwa kutambua mchango wake mkubwa ikiwemo kutokata tamaa alipokuwa akishambuliwa na wadau waliokuwa wakipinga kuanzishwa kwa mfuko huo.

 Ntukamazina (kushoto akipongezana na Humba baada ya kukabidhiwa tuzo
                                 Picha ya pamoja ya mashujaa wa mfuko huo waliokabidhiwa tuzo
 Wageni waalikwa wakiwemo viongozi wa dini, wakipata maelezo kuhusu mfumo wa kisasa wa kuhifadhi mafaili ya wateja wa NHIF
 Wageni waalikwa wakioneshwa jinsi mafaili yalivyopanwa kwa mpangilio mzuri
 Wageni waalikwa wakiangalia mafaili yanayoandaliwa kutunzwa kwa njia ya kisasa
                     Mafaili yakipangwa vizuri ili yahifadhiwe kisasa zaidi
Posted by MROKI On Monday, March 19, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo