HATIMAYE chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)Kwa jimbo la Arumeru kimefanikiwa kupata mgombea ubunge,Joshua Nassari ambapo amefanikiwa kupata kura 805 sawa na asilimia 90.6 ya kura 888.
Akitangaza matokeo hayo kamanda wa oparesheni ya uchaguzi taifa Bw John Mrema alisema kuwa Mgombea huyo amepata kura nyingi sana na kuwaacha wagombea wenzake saba akiwemo aliyehama chama cha mapinduzi baada ya kuambulia kura 22 kwenye kinyang’anyiro cha kura za maoni.
Bw Mrema aliwatanga wagombea wengine kuwa ni pamoja na Bi Anna Mbwira ambaye alipata nafasi ya pili kwa kura 25 sawa na asilimia 2.56 wakati wa tatu ni Bi Rebecca Magwisha ambaye alipata kura 12 sawa na asilimia 1.4
Wengine ni Bw Samwel Shami ambaye naye aliambulia kura 10 sawa na asilimia 1.1 wakati Mgombea Anthony Musani alipata kura 8 sawa na asilimia 0.9 na nafasi ya mwisho ilishikwa na Yohana Kimuto ambaye
alifanikiwa kupata kura 6 sawa na asilimia 0.6
“kwa sheria iliopo na kwa mujibu wa matokeo haya ambayo pia kura sita ziliharibika sasa namtangaza Bw Nassari kuwa ndiye atakayetuwakilisha katika uchaguzi wa jimbo letu la Arumeru Mashariki kwa hivyo
ushirikiano ni muhimu sana””alisema Bw Mrema.
Pia katika Matokeo hayo wagombea wote sita ambao walishindwa katika mchakato huo walisema kuwa kwa sasa wana nafasi kubwa sana ya kuweza kusaidiana ili jimbo liweze kurudi ndani ya chama hicho kwa kuwa wana uwezo wa kuwa na mgombea ndani ya chama hicho.
Akiongea mara baada ya kushindwa katika mchakato huo lakini bado ana nafasi kubwa sana ya kuweza kuelezea umma juu ya chama cha mapinduzi kwa kuwa chama hicho mara nyingi sana kimeonekana kukuika hata maadili ya mtanzania
Bw Musani alisema kuwa bila kuogopa kitu chochote hataelezea hadharani maovu ya CCM ambayo yanafanyika ikiwa ni pamoja na kufichua mbinu mbalimbali ambazo zinafanywa na chama hicho hasa katika nyakati za uchaguzi.
Kwa Upande wake Katibu mkuu wa chama hicho cha chadema Dkt Wilboard Slaa alisema kuwa mpaka sasa kutokana na vijiji 86 kuikubali Chadema ni wazi kuwa jimbo hilo lipo kwao kwa maana hiyo wanasubiri kumupisha Bw Nassari.
Dkt Slaa alisema kuwa mpaka sasa chama chake kimejiwekea utaratibu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanachafua hali ya hewa ndani ya jimbo la Arumeru Mashariki, ambapo kila nyumba itapepea bendera ya Chadema.
“”Nitahakikisha kuwa ili zoezi linaenda vema na pia msije mkaja kwangu mkasema kuwa mmeibiwa kura mimi sitaweza kuwasikiliza ila nitawauliza maswali hakikisheni kuwa hamuibiwi kura na kila nyumba inatakiwa
kuppeea bendera ya Chadema tena mpya kabisa na mimi nitasimamia hili zoezi”alisema Dkt Slaa.
Naye Mshindi ambaye ni Nassari alisema kuwa mara baada atakapoingia Bungeni atahakikisha kuwa anarudisha ubunge kwa wanananchi ikiwa ni pamoja na kujinyima hata kwa posho zake ili kuwarudishia wananchi maendeleo.




0 comments:
Post a Comment