Nafasi Ya Matangazo

March 23, 2012



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliamo TCRA, Prof.John Nkoma amesema bila ya kuwepo kwa ushindani katika vyombo vinavyotoa huduma ya mawasiliano hakuwezi kuwepo kwa udhibiti katika vyombo hivyo.

Amesema kuwepo kwa ushindani katika tasisi hizo kunaweza kumpa mteja kuchagua hudma nzuri aipendae na pia kuna uwezo mkubwa wa upunguaji wa bei katika makampuni hayo ili kuvuta wateja wengi zaidi .

Mkurugenzi huyo amesema hayo alipokua akikaribisha kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi ilipofika katika ofisi kuu ya TCRA jijini Dar es salaam kwa lengo la kujifunza mambo mbali mbali yanayohusu mawasiliano.

Aidha alisema kazi kubwa ya mamlaka hiyo ni kutoa leseni kwa kampuni ambazo zinajishulisha na utoaji huduma ya mawasiliano  na kufuatilia leseni hizo kama zinatumika  ipasavyo.

Aidha alisema hivi sasa mamlaka yake imo katika mchakato wa kuandaa miradi miwili ambayo ni kutafuta utaratibu mzuri wa anuni ya maakazi ambao utamuezesha mtumiaji wa posta ajulikane hadi sehemu anayoishi na inapotokea ajali ya moto au mgonjwa iwe rahisi kujulikana alipo.

Akizungumzia mradi wa pili mkurugenzi mkuu huyo amesema mamlaka kwa kushirikiana na taasisi nyengine ambazo zinajishughulisha na utoaji huduma ya mawasiliano zimo mbioni kutoka katika mfumo wa analogi na kuingia digital jambo ambalo litaifanya Tanzania iwe kati ya nchi zenye kutumia teknolojia ya kisasa katika mawasiliano.

Hata hivyo aliifahamisha Kamati hiyo kuwa Mamlaka   inajitahidi kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria zilizopo za mawasiliano ili wateja wao wapate hudma zilizo bora na salama.

Aidha alisema ingawa TCRA ina mafanikio makubwa lakini bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya wizi wa mawasiliano pamoja na  wizi wa pesa katika simu ambapo alisema Mamlaka yake tayari imeshajipanga katika kudhibiti suala hilo na atakae kamatwa  hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Hata hivyo alisema TCRA ina ndoto kubwa ya kupanua mtandao wa mawasiliano kwa faida  na maslahi ya watanzania wote ili waweze kwenda sambamba na sayansi na teknolojia.

Katika kikao hicho wajumbe wa Kamati walipata fursa  ya  kupewa elimu ya kutoka katika mfumo wa kizamani wa analogi na kuingia katika mfumo wa kisasa wa digital pamoja anuani za makazi ambapo wajumbe hao walisema wamefaidika na elimu waliyoipata na kuwa wawakilishi wazuri kwa wengine .

Aidha mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Mawasiliano na Ujenzi Makame Mshimba Mbarouk amesema ni vyema Mamlaka ikaharakisha miradi hiyo kwani itakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wote wa nchi hii.

Kwa upande wake kiongozi wa msafara huo mkurugenzi utumishi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliani Rajab Yakoub Uweje amesema kuwepo kwa ziara kama hizo kwa Kamati za Baraza la Wawakiliishi zimekua zikirahisisha kufikisha ujumbe harakaa kwa wananchi kwa kile Wawakilishi wao wanachojifunza kutoka taasisi mbali mbali za umma.

Aidha amesema licha ya Kamati hizo kujifunza lakini pia wanapata changamoto kubwa kwakile wanachokiona katika maeneo wanayotembelea  na kuisukuma serikali ili nayo iweze kufikia hatua kama hizo.
Posted by MROKI On Friday, March 23, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo