Baadhi ya waandishi wa habari wa jijini Mbeya wakishindana kutambua ladha ya bia za kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Baadhi ya wanahabari wakichungulia sehemu inayotumika kupikia bia katika kiwanda cha bia cha Mbeya. Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mbeya, Calvin Martine akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya, kuhusu uzalishaji wa bia walipotembelea kiwanda hicho, mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya waandishi wa habari wa jijini Mbeya wakitembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kilichopo Iyunga jijini humo mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mbeya, Calvin Martine akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya, kuhusu uzalishaji wa bia walipotembelea kiwanda hicho, mwishoni mwa wiki.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), akizungumza na Baadhi ya Waandishi wa habari wa Jijini Mbeya wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa kampuni ya uzalishaji vileo ya TBL wakati wa kubaini ladha halisi ya vileo vinavyozalishwa na kampuni hiyo.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi akimkabidhi katoni ya bia aina ya Castle Lager, mwandishi wa habari wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Steve Jonas ambaye alikuwa ni mshindi wa pili kati ya washindi watatu waliofanikiwa kubaini ladha halisi ya bia zinazotengenezwa na kampuni hiyo Jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Habari Leo Joachim Nyambo akipokea zawadi ya katoni ya Bia aina ya Ndovu kutoka kwa Meneja Uhusiano na Mawasiliano Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi baada ya kuibuka mshindi wa kubaini ladha halisi ya aina ya vileo vinavyotengenezwa na kampuni ya Bia ya TBL.Mashindano hayo yaliyohusisha wannahabari wa mkoa huo yalifanyika mwishoni mwa wiki.
Mshindi wa kwanza wa uonjaji ladha halisi za Bia zinazotengenezwa na Kampuni ya TBL Mbeya ambaye ni mwandishi wa habari wa Chanel Ten Saada Matiku akipokea katoni za Bia kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha Bia mkoani Mbeya Calvin Martin, Matiku alizawadiwa katoni tatu za Bia.
0 comments:
Post a Comment