Bw Wens Mushi ambae ni Kaimu Naibu Mhariri wa The Guardian akitoa maelekezo kwa Rais wa Airtel Afrika kitengo cha mawasiliano (alieshikilia gazeti) huku Bw Alexander Doll Mkurugenzi mkuu wa Hill+Knowlton Strategies (wapili toka shoto) toka kampuni maalum ya Mahusiano ya Airtel Afrika akifuatilia kwa undani zaidi. Anaefuata ni Mhariri mtendaji wa gazeti la Nipashe Bw Jesse Kwayu pamoja na wadau wa Airtel nchini Tanzania
Bw, Isack Gamba ambae ni kiongozi wa vipindi Radio one na Mtangazaji wa ITV akiwaelezea jinsi wanavyofanya vipindi na kushirikisha wasikilizaji live katika studio za Radio one sterio jijini dar.
Kutoka shoto ni Makamu wa Rais wa Airtel Afrika kitengo maalum cha mawasiliano Michael Okwiri akipokelewa na Bi. Joyce Luhanga Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha IPP (kati) mara baada ya kuingia katika ofisi kuu za IPP Mikocheni jijini Dar leo. Mwishoni ni kiongozi wa vipindi Radio one na Mtangaza wa ITV Bw, Isack Gamba akiwaongoza pia.
Kulia ni Nasa Kingu Mkuu wa Vpindi wa East Afrika TV/ Radio akiwapokea na kutoa maelezo jinsi wanavyofanya shughuli za habari katika ofisi za East afrika TV/Radio.
====== ====== ===== =======
Rais wa Airtel Afrika kitengo cha Mawasiliano atembelea Tanzania
• Apongeza juhudi za wanahabari nchini Tanzania
• Ahaidi Airtel itakuwa mstari wa mbele kushirikiana na wanahabari
katika mawasiliano
• Apongeza juhudi za wanahabari nchini Tanzania
• Ahaidi Airtel itakuwa mstari wa mbele kushirikiana na wanahabari
katika mawasiliano
Rais wa Airtel Afrika katika kitengo maalum cha mawasiliano kwa umma leo amepongeza juhudi za wanahabari nchini mara ya kutembelea baadhi ya vyombo vya habari Tanzania ikiwemo IPP media na Mwananchi Communication ikiwa ni ziara ya siku mbili ya aliyojiwekea ili kujionea mambo mbalimbali katika ulimwengu wa Habari na Mawasiliano nchini.
Akiongea wakati wa ziara hiyo akiwa na wadau mbalimbali na wanahabari,Rais wa Airtel Afrika bw, Michael Okwiri alisema “Nimegundua Tanzania kuna maendeleo mazuri sana hasa ukiangalia mitambo na vyombo vya habari kwa kweli vinaonyesha kupiga hatua kwa kiwango”Vilevile nawapongeza sana wanahabari (Journalists).kwa juhudi zenu za kutafuta habari na kuziwahisha kuzichapa kwa muda wa siku pamoja na mambo mengi, kwa kweli ni juhudi inayohitajika kukamilisha mambo haya mapema ili wasomaji wapate taarifa inayoendana na muda.
Kwa upande wetu Airtel naomba niwashukuru wanahabari wote kwa ujumla nchini Tanzania hasa mnaoshirikiana nasi Airtel kuhakikisha huduma ya mawasiliano ya uhakikika inawafikia wananchi kwa kupitia baadhi ya habari zinazochapwa na kusambazwa nchini na vyombo vyenu. Airtel tunaahidi ushirikiano wa kutosha katika mawasiliano ili tuweze kutimiza dhamira yetu ya Uhuru wa kuongea nchini kote” alimaliza kusema bw. Okwiri.
0 comments:
Post a Comment