Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, Waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kushoto) akibadilishana hati ya mkataba wa Makubaliano ya Udhamini wa Miss Tanzania na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Fimbo Butala leo hii muda mfupi baada ya kutiliana saini mkataba huo utakao gharimu kiasi cha zaidi ya Tsh Milioni 700 ambapo mkataba huo utadumu kwa miaka 3.
REDD’S ORIGINAL MDHAMINI MKUU WA MISS TANZANIA 2012.
Dar es Salaam, FEBRUARY 15, 2012:
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo imetangaza rasmi kuchukua nafasi ya “Mdhamini Mkuu” wa shindano kubwa kabisa la urembo hapa nchini lijulikanalo kama “Miss Tanzania”.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, meneja masoko wa TBL Bw. Fimbo Butallah alisema; Redds Original, leo inatangaza kuwa ndio wadhamini wakuu wa mashindano ya urembo Tanzania, yanayojulikana kama “Miss Tanzania”. Kwa udhamini huu, mashindano haya sasa yatajulikana kama “REDDS MISS TANZANIA 2012”. Kwa miaka kadhaa sasa Redds Original imekuwa ikishiriki katika mashindano haya kama mdhamini mwenza, yaani “Kinywaji rasmi cha Miss Tanzania”. Hivyo leo tunapiga hatua nyingine kubwa katika historia ya tasnia hii ya urembo hapa nchini kwa kuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya Miss Tanzania.
Katika kuonesha kuwa Redds Original, imedhamiria kwa dhati kuendeleza tasnia hii, leo tumesaini mkataba wa udhamini wa mashindano haya kwa kipindi cha miaka mitatu, yaani 2012 hadi 2014. Hii inawahakikishia wapenzi na mashabiki wa mashindano haya kuwa wataendelea kushuhudia mashindano haya na kuburudika na kinywaji cha Redds Original kwa kipindi chote hiki. Alisema Butallah.
Nae Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Bi. Victoria Kimaro alisisitiza juu ya udhamini wa mashindano haya kuanzia ngazi za chini hadi ngazi ya Taifa. Udhamini huu mkubwa wa mashindano ya Miss Tanzania unajumuisha udhamini tutakaotoa katika maeneo mbali mbali kwa ngazi za vitongoji hadi Taifa. Tunawaahidi mashabiki wote wa mashindano haya na wadau wa tasnia ya urembo kujiandaa kwa burudani ya hali ya juu.
Akizungumzia udhamini huo, Mkurugenzi wa LINO Agency waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Bw. Hasim Lundenga alisema; Kwa niaba ya kamati ya Miss Tanzania napenda kutoa shukurani za dhati kwa TBL kupitia kinywaji chake cha Redds Original kwa udhamini huu, na tunatangaza rasmi kuwa mashindano haya sasa yataitwa “Redds Miss Tanzania’. Kitu kikubwa tunachowashukuru wadhamini wetu ni mkataba ambao tumesaini hii leo, ukituhakikishia udhamini wa mashindano haya kwa miaka mitatu.
Kwa mara nyingine tunawapongeza zaidi Redds original kwa kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza tasnia hii ya urembo hapa nchini. Tumekuwa nao bega kwa bega kwa miaka kadhaa sasa, na haiwezekani ukazungumzia tasnia ya urembo hapa nchini bila kuitaja Redds Original. Alisema Lundenga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, Waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kushoto) akitiliana saini na kataba wa udhamini na shindano la Miss Tanzania na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Fimbo Butala leo hii
Mwenyekiti wa Miss Tanzania, Prashant Patel (kushoto) akiwa na Hashim Lundenga.
Meneja wa Kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro akifafanua jambo juu ya udhamini huo na Kulia ni Miss Tanzania 2011, Salha Izrael.
Hasim Lundenga akifafanua jambo
0 comments:
Post a Comment