Tunapenda kuwatangazia Kifo cha Ndugu. Amani Mroki Majengo (pichani) kilichotokea leo Saa nane mchana Katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi.
Mipango ya Mazishi inafanyika Nyumbani kwa Marehemu Ugweno Msangeni jirani “KANKUNI” na kwa dada wa marehemu Segerea jijini Dar es Salaam.
Marehemu Mroki, alikuwa akisumbuliwa na saratani ya tumbo na ameugua kwa muda mfupi. Wakati wa uhai wake aliwahi fanya kazi Ushirika TRC katika mikoa ya Kagera0 na Kilimanjaro na hadi mauti yanamkuta alikuwa akifanya kazi katika Kampuni ya Udalali ya Majembe Action Mart Kanda ya Arusha.
Mazishi ya Mpendwa wetu, Mroki yanataraji kufanyika Jumamosi hii Ugweno Msangeni, wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
Rest in peace AMANI Mroki tulikupenda ila Mungu kakupenda zaidi MUNGU awape moyo wa subira ndugu na jamaa wote ameni .Nusra msangi
ReplyDeletePoleni sana na matatizo yaliyowafika. Mungu amlaze marehemu mahala pema peponi.
ReplyDeletePia naomba nitoe tu ushauri, matangazo ya vifo yasianze kwa "Tunapenda", nadhani "Tunasikitika kutangaza" inafaa zaidi.
Hakika Wote ni waja wa Allah na kwake tutarejea!!
ReplyDeleteBwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake litukuzwe.
Tulimpenda sana lakini Bwana amempenda zaidi
Mwenyezimungu amlipe kwa mema yake yote na amsamehe makosa yake yote!! Ameen;
Prof Jafari R Kideghesho