Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiongoza maanadamano ya uzinduzi wa muongo wa usalama barabarani na huku akisalimiana na wananchi waliokusanyika pembezoni na Makamo wa Kwanza wa Rais maalim Seif Shariff kama wanavyoonekanwa pichani,maandamano hayo yalianzia Bwawani yakielekea Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,alipofika kuwafariji wagonjwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, waliopata ajali mbali mbali, ikiwa ni katika uzinduzi wa Muongo wa Usalama barabarani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein akivishwa Beji kuashiria Usalama Barabarani na Rais wa Kitengo cha Usalama Barabarani wa Oman Balozi Wahid Alkharous katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar leo katika hafla ya uzinduzi wa Taifa wa Usalama Barabarani .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein akitoa hotuba yake kuhusu Usalama Barabarani katika uzinduzi wa Taifa wa Usalama Barabarani uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar
Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Zanzibar Hamad Masoud Hamad akitoa hotuba kuhusu Usalama Barabarani katika uzinduzi wa Taifa wa Usalama Barabarani kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Rais Shein kuhutubia katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein akimfariji Mgonjwa Yassir Yussuf ambaye amepata ajali ya Pikipiki na kulazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar katika Uzinduzi wa Taifa wa Usalama Barabarani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein akiwa katika matembezi pamoja na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad kulia kwake,kushoto kwa Rais ni Rais wa Kitengo cha Usalama Barabarani wa Oman Balozi Wahid Alkharous walipokuwa wakielekea Hospitali ya Mnazi Mmoja ili kuwakagua wagonjwa waliokuwa wamepata ajali
0 comments:
Post a Comment