Nafasi Ya Matangazo

December 29, 2011


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biasha Bi Joyce Mapunjo( Alieketi Katikati) akiwa katika picha ya  pamoja na Wadau wa Mkutano wa kuandaa Sera ya Taifa ya Miliki Ubunifu uliofanyika Hoteli ya Blue Pearl Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi Joyce Mapunjo amewataka wadau wa maandalizi ya sera ya Taifa ya Miliki inakidhi mahitaji ya nchi ya kwa kujenga msingi wa matumizi ya Miliki ubunifu ili kuchangia kikamilifu katika kufikia lengo la Taifa la Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025

Mh Mapunjo ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati ikifungua mkutano waWadau katika kuandaa sera hiyo, mkutano uliofanyika katika Hotel hya Blue Pearl.

“Ubunifu ni nyenzo muhimu sana ya kuongeza ubora wa bidhaa na huduma zinazozalishwa kwa gharama nafuu. Sera ya Taifa ya Miliki Ubunifu itasaidia kufikiwa kwa malengo ya 2025 ikiwemo kupunguza umasikini nchini. Kufanikishwa kwa lengo hili la kitaifa kutapelekea ukuaji wa uchumi wetu kwa kiwango kati ya 8% hadi 10% katika sekta ya kilimo sambamba na sekta ya viwanda inayotegemewa na caribú 70% ya Watanzania.

Hii itawezekana tu iwapo kutakuwa na maendeleo ya kibiashara na uhamasishaji wa matumizi ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu vya ndani katika masoko ya maeneo EAC na SADC pamoja na masoko mengine ya kimataifa ambako kuna ushindani mkubwa.” Amesema Mapunjo.

Bi Mapunjo ameongeza kuwa, Tanzania imepiga hatua kubwa ya ubunifu katika maeneo nyeti ya kiuchumi kama vile kilimo, kwa hiyo ipo haja ya kuhakikisha uvumbuzi huo unalindwa ipasavyo. Ni muhimu pia kulinda mali asili zetu kama vile utamaduni, na maeneo ya kijiografia. Maeneo mengine yanayohitaji kulindwa ni pamoja na muziki, na sanaa.

Tanzania ni mjumbe wa WTO katika kundi la nchi masikini (LDCs) ambapo inayo fursa ya kufaidika na makubaliano mbalimbali ya kimataifa ambayo hupatikana tu pale ambapo nchi husika itazingatia utekelezaji makini na wa kimkakati wa Sera ya Taifa ya Miliki Ubunifu.

Ubunifu kuhakikisha sera hiyo
Posted by MROKI On Thursday, December 29, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo