Nafasi Ya Matangazo

November 14, 2011

KAMPUNI inayoongoza ya usimamizi wa vyombo vya habari katika nchi za Afrika Mashariki, Push Observer imemtangaza gwiji la sekta hiyo Duniani, Joe Taylor (pichani) kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wake.
 
Akizungumza jijini jana, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Push Observer,  Omari Salisbury  alisema kuwa  hatua ya kumwajiri Taylor imetokana na historia yake nzuri katika sekta hiyo nchini Marekani na kampuni yao inataka mafanikio makubwa katika sekta hiyo katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.
 
Salisbury alisema kuwa Taylor ambaye kwa sasa amekwisha anza kazi, alikuja nchini kwa mara ya kwanza mwezi Septemba na kuendesha ‘semina’ kwa wadau mbali mbali kwenye hotel ya Sea Cliff na kuwafumbua macho wadau wengi wa sekta hiyo.
 
Alisema kuwa wanaamini kuwa ujio wake na kufanya kazi na kampuni hiyo kutawawezesha kupata maendeleo makubwa huku wakitoa huduma bora zaidi katika Nchi za Afrika Mashariki.
 
“Lengo ni kupata maendeleo makubwa katika sekta ya usimamizi wa habari, tumeamua kuajiri mtu bora kabisa kwa lengo la kutoa huduma bora kabisa, naamini wadau wetu wakiwemo waandishi wa habari watapata kile wanachokihitaji katika kazi zao,” alisema Salisbury.
 
Alisema kuwa Taylor ni kiongozi bora na amekuwa katika fani hiyo kwa miaka 30 nchini Marekani. Kabla ya kujiunga na Push Observer, alikuwa mkurugenzi wa kampuni ya VMS na mwaka 2009  walifanikiwa kushinda tuzo ya mwaka ya  Innovation (Innovation  of the Year Award) na mwaka huo huo wakashinda tuzo ya Cost Saving Award.
 
Talylor vile vile amewahi kushika nyadhifa mbali mbali ikiwa pamoja na makamu wa Rais wa kampuni ya Broadcast Monitoring for Medalink na Rais wa Broadcast News Mid-America,Oklahoma.
 
Taylor alisema kuwa amefurahi kujiunga na Push Observer na kufanya kazi Tanzania na anaamini kuwa kampuni hiyo itafika mbali kwa kupata maendeleo makubwa.
Posted by MROKI On Monday, November 14, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo