Nafasi Ya Matangazo

November 26, 2011

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwapungia mikoni mashabiki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii,  Mara baada ya kuzindua rasmi michuano ya TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 ambapo leo michuano hiyo imekutanisha timu za Tanzania Kilimanjaro Stars na Timu ya taifa ya Rwanda Amavubi,  mpira umekwisha na timu ya Rwanda imeifunga Kilimanjaro Stars  goli 1-0 , katika picha kulia  anayecheka ni Rais wa TFF na Shirikisho la Vyama vya michezo Afrika Mashariki na kati CACAFA Leodger Tenga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Bw. Richard Wells  na  Teddy Mapunda (kulia)Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo wakiwapungia mkono  Mashabiki waliojitokeza katika uzinduzi huo wa Michuano ya TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii
Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars Mbwana Samatta  katikati akipiga mpira wa kichwa langoni mwa timu ya Amavubi huku mabeki wakijaribu kuzuia mpira huo usilete madhara golini mkwao.
Mashabiki wa timu ya Kilimanjaro Stars wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Mashabiki wakifuatilia kwa karibu mpambano huo kati ya Kilimanjaro Stars na Timu ya taifa ya Rwanda wakati wa mchezo wao wa kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Kikundi cha Sarakasi kikifanya vitu vyake wakati wa mapumziko ya mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries (SBL) akihojiwa na mtangazaji wa Televisheni ya Super Sport wakati wa mapumziko ya mchezo kati ya Kilimanjaro Stars na Rwanda.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Mizengo Pinda katikati akiwa tayari kwa kukagua timu ya kisha kuzindua mashindano hayo ambayo yalianza jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadick na kutoka kushoto ni Dr. Fenella Mukangara Naibu Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo, Dr. Emmanuel Nchimbi Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo na Leodger Tenga Rais wa Shirikisho la vyama vya michezo Afrika Mashariki na kati CECAFA na TFF.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Mizengo Pinda wa pili kutoka kushoto akiwapungia mikono mashabiki wa soka mara baada ya  kuzindua mashindano hayo ambayo yalianza jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kushoto  ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadick na wa pili  kutoka kulia ni Dr. Fenella Mukangara Naibu Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo, Richard Wells Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) na Leodger Tenga Rais wa Shirikisho la vyama vya michezo Afrika Mashariki na kati CECAFA na TFF.
Kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda Amavubi kikiwa katika picha ya pamoja.
Kikosi cha timu ya taifa yaTanzania Kilimanjaro Stars  kikiwa katika picha ya pamoja.
Posted by MROKI On Saturday, November 26, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo