Nafasi Ya Matangazo

November 03, 2011

Na Mwaandishi wetu
KAMPUNI ya bia ya East African Breweries Limited (EABL) itaanza kuuza hisa zake inazozimiliki katika Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) leo.

Taarifa iliyotelewa na Kampuni hiyo jana ambaye haikutaja bei za hisa ilisema kampuni hiyo ilipata idhini ya mamlaka husika ya Capital Markets and Securities Authourity (CMSA). Tarifa hiyo ilisema bei ya hisa hizo itatajwa mara tu bada ya kuanza kwa zoezi .

EABL ni miongoni ya kampuni zilizoorodeshwa kwenye masoko ya hisa mbali mbali hapa Afrika Mashariki ikiwa kwenye Soko La Hisa la Dar es Salaam (DSE), Soko la Hisa la Uganda (USE) na Soko la Hisa la Kenya (NSE).
Rekodi zinaonyesha kuwa EABL ilinunua hisa asilimia 51 katika kiwanda cha Serengeti Breweries Limited (SBL) baada ya kuruhusiwa kwa masharti na Tume ya Ushindani wa Kibishara (FCC), masharti hayo yakiwa pamoja na kuuza hisa zake asilimia 20 kwenye kampuni ya TBL.

“Baada ya mashauriano na Tume ya Ushindani Juni 22 mwaka huu kampuni ilikubali kuwajibika kwa kushindwa kutekeleza sharti hilo. EABL iliomba radhi kutokana na kushindwa kutekelezwa kwa sharti hilo na kuahidi kuwa tatizo hilo lingemalizika, ” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa EABL, Seni Adetu katika tariifa iliyotelewa Jumapili.
Wadadisi wa maswala ya kiucumi wanasema lengo la kamuni hiyo ni kuwa minongoni ya kampuni kubwa za bia hapa Afika Mashariki ikiwa na kuteka soko hilo.
Posted by MROKI On Thursday, November 03, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo