Mmoja wa majeruhi wa risasi za polisi katika vurugu za Mwanjelwa leo, Abel Mwalukali akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kupigwa risasi kwenye mkono.
| Baadhi ya wamachinga wakiwa wamelipindua gari yaina ya toyota na kusimama juu yake huku wakitamka maneno makali kwa polisi na jiji la mbeya kwa kuwanyanyasa katika biashara zao |
| Moja ya mabango waliyobeba wamachinga hao |
| Wamachinga wakiwazomea polisi eneo la kabwe |
| Maduka yote eneo la mwanjelwa mpaka uyole yamefungwa |
| Moja ya gari lililobinuliwa na kuwekwa katikati ya barabara ya mbeya tunduma |
| Huu ndiyo mtaa wengi huuita mtaa wa kasisi uliyosababisha vurugu zote kati ya wamachinga na askari wa jiji |
| Mmachinga akiwarushia jiwe kwa kutumia manati yaani ni hatari tupu |
| Askari wa kutuliza fujo naye akiwarushia bomu la machozi wamachinga wanaoandamana |
| RISASI ZA MOTO NAZO ZIMETUMIKA KATIKA TUKUKIO HILI |
| MABOMU YA MACHOZI NDIYO USISEME KILA MAHALI YAMETAPAKAA |
| Mwenye kofia haya mwenye supu haya kila mmoja alikua anaokoa uhai wake |
| Raia wema wakivukishwa barabara eneo la mapambano maeneo ya kabwe |
| Moja ya gari lililopasuliwa kioo na baruti |
| Wamachinga wakishangilia baada ya kuwazidi polisi nguvu |
| Nivurugu tupu maeneo ya soweto jijini mbeya |
| Wamachinga wakichochea moto wa matairi katikati ya barabara ya mbeya na tunduma. |





0 comments:
Post a Comment