Miss Mtwara 2011, Rahma Swai (21) pichani amefariki dunia hii leo mjini Mtwara.
Taarifa iliyozifikia Blogu hii kutoka kwa marafiki wa karibu na marehemu zinasema Marehemu Rahma alifikwa na umauti baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa tumbo jana nakufikishwa katika Hospitali ya Mtwara kwa matibabu na ilipofika alfajiri ya leo Oktoba 18, akapoteza maisha.
Aidha marafiki hao wamedai kuwa Mwili wa Marehemu Rahma unataraji kufikishwa nyumbani kwao leo Changanyikeni Jijini Dar es Salaam tayari kwa mipango ya mazishi.
Rahma pia alikuwa ni Miss Kanda ya Mashariki Namba 4 katika shindano lililofanyika mjini Morogoro mwaka huu.
Blogu ya Father Kidevu ambayo ilikuwa mmoja wa wadhamini wa Shindano la Kanda ya Mashariki inatoa pole kwa familia ya marehemu ndugu jamaa na marfiki kwqa kufikwa na msiba huo mkubwa katika kipindi hiki ambacho Jamii ilikuwa inautegemea sana mchango wake katika tasnia ya urembo nchini.
Mungu ampe Hifadhi ya Milele Amina.
mmhhh poleni sana wana familia na tanzania kw ajumla.
ReplyDeletejanet wa Dar.