Mkoa waIringa mbali na kuwa miongoni mwa mikoa nchini ambayo huzalisha sana mazao ya chakula hasa Mahindi, lakini pia mkoa huu umekuwa mbele kwa uzalishaji wa mboga mboga kama nyanya na vitunguu. Katika kipindi chote cha mwaka zao la nyanya limekuwa likipatikana katika maeneo mengi ya mji mkoa huo hasa kando kando ya barabara kuu ya Iringa Mbeya au Iringa Morogoro.
Pichani ni wafanya biashara wa nyanya na vitunguu katika eneo la Ilula mkoani Iringa wakiwahudumia wasafiri waliosimama kwa muda na gari ili kujipatia mahitaji yao katika eneo hilo ambalo linazalisha zao hilo kwawingi, na idadi kubwa imekuwa ikisafirishwa jijini Dar es Salaam. Ndoo moja ya nyanya kama hiyo inauzwa kati ya Sh 4,000/= na 3,000/= huku vitunguu vikiuzwa kati ya sh 7,000/= na 6,500/=.
0 comments:
Post a Comment