MPENDWA MAMA YETU JOYCE PETER NKURLU, ILIKUWA SIKU, MWEZI NA HATIMAYE MIAKA MIWILI SASA TANGU UTUTOKE TAREHE 12/10/2009 KATIKA DUNIA HII. LAKINI TUNAFARIJIKA KWA SABABU TUNA AMANI UKO PAMOJA NASI KIROHO SIKU ZOTE.
MAMA HAKUNA SIKU IPITAYO KWETU BILA KUKUMBUKA KWA UPENDO, UKARIMU NA KUJALI KWAKO KATIKA KUTULEA NA KUTUUNGANISHA SISI WANAO NA FAMILIA PAMOJA. HAKIKA UPENDO WAKO UMEKUWA DIRA NA NURU KATIKA MAISHA YETU.TUNAENDELEA KUKUOMBEA NA TUNAENDELEZA YALIYO MEMA KWA WAJUKUU ZAKO UPUMZIKE KWA AMANI.
DAIMA UNAKUMBUKWA NA WATOTO WAKO: ATUZA, ANGAZA, AMANI, NZIGIA, MATINA NA MASALA. WAJUKUU ZAKO AMANI, VANESSA-SALOME NA NGULLA, BILA KUSAHAU MAMA YAKO, DADA NA KAKA ZAKO WOTE, NDUGU JAMAA NA MARAFIKI PAMOJA NA WAUMINI WENZAKO. DAIMA TUTAKUKUMBUKA MILELE.
MAMA TULIKUPENDA SANA, LAKINI MUNGU BABA WA MBINGUNI ALIKUPENDA ZAIDI.BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE MILELE.
0 comments:
Post a Comment