Nafasi Ya Matangazo

October 14, 2011

Afisa  Mtendaji wa kata ya Msolwa Ujamaa mkoani Morogoro Kilombero  Bw Edward Tesha akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara wa mawasiliano wa kampuni ya simu ya Airtel uliozinduliwa leo ili kuboresha zaidi mawasiliano mkoani Morogoro kilombero, mnara huu  utatoa mawasiliano bora kwa wakazi wateja wa Airtel wa vijiji vya Msolwa stesheni, Kidatu, Sanje, Mkula, Sumbugulu, Nyange, Magombera, Miwangani pamoja na jirani zao wote.
Toka kulia ni Meneja mauzo wa kanda ya kati wa Airtel Bw Aluta kweka akikabidhi zawadi ya mbuzi kwa bw Fidelis Mkwenya (kati aliyevalia jezi ya arsenal) ambae ni kapteni wa timu ya mpira wa miguu wa kijiji cha msolwa ujamaa B mara baada ya timu yao kuibuka washindi wa mchezo maalum ulioandaliwa na Airtel kwa kushirikisha timu ya Msolwa ujamaa A na B na kisha timu ya msolwa B kuibuka washindi kwa bao 4-3 wakati kampuni ya airtel ilipozindua rasmi mnara wa mawasiliano na kuboresha mawasiliano katika vijji vya Msolwa stesheni, Kidatu, Sanje, Mkula, Sumbugulu, Nyange, Magombera, Miwangani pamoja na jirani zao wote.
***************
  • Zaidi ya vijiji kumi mkoani Moro kilombero kufaidi mawasiliano ya  sasa.
Morogoro 13, October 2011 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mwishoni mwa wiki hii imezindua huduma za mawasiliano mjini na vijijini ikiwa ni katika muendelezo wa dhamira yake ya kufikia wanananchi wengi na kuinua shughuli za uchumi nchini.

Akizungumza na wakati wa uzinduzi huo Meneja wa Kanda wa Airtel Bw Aluta kweka alisema "Airtel leo tunazindua na kupanua huduma zetu mkoani Morogoro-Kilombero katika vijiji vya Msolwa stesheni, Kidatu, Sanje, Mkula, Sumbugulu, Nyange, Magombera, Miwangani pamoja na jirani zao wote.

Airtel bado tunaendelea na mchakato wa kupanua mawasiliano kila mahali ili kuhakikisha mwasiliano bora tutakayotoa yatapunguza changamoto zinazowakabili jamii hasa maeneo ya vijijini.

leo hii tumefikisha huduma hii hapa Morogoro vijijini, hii ni wazi kuwa tunaendelea kutekelezaji dhamira ya kuchangia maendeleo ya nchikupitia sekta ya mawasiliano.

Airtel tunaimani kuwa  kuboresha mawasiliano katika vijiji a ni chachu ya kipeeke katika kuchangia maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Posted by MROKI On Friday, October 14, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo