Nafasi Ya Matangazo

October 13, 2011

Jamboree ya hewani ya Kimataifa ya Skauti itafanyika mkoani Arusha tarehe 15 na 16 Oktoba 2011.

Jamboree ya Hewani ni kambi ambayo skauti duniani pote huwasiliana na skauti wengine kwa kutumia vifaa vya mawasiliano [Radio calls] pamoja na mtandao wa Kompyta. [internet]

Hii ni mara ya kwanza kwa Kambi hii kufanyika kitaifa  nje ya mkoa wa D’salaam, Skauti kutoka mikoa mbalimbali nchini wanatakiwa kuhudhuria kambi hii muhimu ambayo pia ni sehemu ya mafunzo kwao.

Jamboree ya Hewani ya Kimataifa ni shughuli ambayo hufanyika kila mwaka mwezi wa Oktoba, na madhumuni  yake ni kuwaweka karibu skauti duniani kote kwa kutumia Mawasiliano ya Radio na mtandao wa Komputa, [internet]

Shughuli hii ambayo hufanyika kwa muda  siku 2 [saa 48] huwapa fursa skauti kubadilishana  ujuzi mbalimbali ikiwa ni pamoja mafunzo ya kiskauti, nyimbo, na michezo mbalimbali. Kupitia kambi hii ya Kimataifa, skauti pia hujifunza lugha mbalimbali za kimataifa.

Mgeni rasmi katika ufunguzi wa kambi hiyo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, na inakadiliwa jumla ya skauti 1000 watahudhuria.

 HIDAN .O. RICCO.
KAMISHNA MKUU MSAIDIZI
MAWASILIANO NA HABARI
CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA.
Posted by MROKI On Thursday, October 13, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo