Jeshi la Polisi nchini (PT) kupitia Inspekta Generali wake Said Mwema imetangaza dau la Shilingi Milioni 5 kwa mtu yeyote atakae fanikisha kupoatikana kwamtu aliye mjeruhi mtoto Adam Robert (14) ambaye ni Albino huko Geita ambapo mtu asiyejulikana alimvamia mtoto huyo na kuanza kumkata kata mikono na kisha kutoweka na vidole vya Albino huyo.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia mwishoni mwawiki katika Kijiji cha Nyaruguguna, Kata na Tarafa ya Nyang’hwale ambapo mlemavu huyo, Adam Robert (14), mwanafunzi wa darasa la nne, alivamiwa na kukatwa mkono wa kulia na kisha kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kushoto.
hii sio njia sahihi ya kukabiliana na vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi. madau mangapi yatatangazwa?
ReplyDelete