Mvua ya leo imeweza kuzua kizazaa baadhi ya sehemu hasa maeneo ya Mabibo kwa kusababisha nguzo moja, kuilalia nguzo nyingine. Nguzo hiyo ni miongoni mwa nguzo ambazo Tanesco wamekuwa wakiziweka sasa na tayari baadhi ya watu wanasema zimeshaanza kupitisha umeme.
Wananchi wa maeneo hayo ya Mabibo maeneo ya Makutano, wamesema wanaomba Tanesco wafanye haraka kwenda kuinua nguzo hiyo, kwakuwa umeme bado unaendelea kutumika, hivyo ni hatari sana kwakuwa nguzo hiyo haijajishika vizuri eneo hilo jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya wakazi wa hapo, kwakuwa mvua zinaendelea kunyesha.
Bongo5
Posted by MROKI
On Saturday, October 01, 2011
No comments
0 comments:
Post a Comment